May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Raila amtembelea Rais Samia, wajane mama Janeth Magufuli, Anna Mkapa

Spread the love

 

KIONGOZI mkuu wa Cha cha upinzani nchini Kenya (ODM), Raila Odinga, jana tarehe 25 Agosti, 2021 amefanya ziara ya siku moja nchini Tanzania na kuzungumza na Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na wajane wa marais wastaafu Mama Janeth Magufuli pamoja na Anna Mkapa. Anaripoti Mwandishi wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Odinga alikuwa njiani kutokea Zambia ambako alikuwa ameungana na viongozi kadhaa wa Afrika kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais wa Zambia Hakainde Hichilema.

Kupitia ujumbe alioubandika katika akaunti yake ya Twitter, waziri huyo mkuu wa zamani wa Kenya alisema kuwa mazungumzo kati yake na Rais Samia  Ikulu yalihusu namna ya kuimarisha ujenzi wa miundombinu katika eneo zima la Afrika Mashariki.

“Vile vile, tulijadili njia mbalimbali za kuimarisha uchukuzi wa majini katika ukanda wa Afrika Mashariki kupitia Ziwa Victoria,” alisema.

Baadaye kiongozi huyo, ambaye ni Mjumbe Mkuu wa Umoja wa Afrika (AU) kuhusu miundombinu, aliwatembelea wajane wa waliokuwa marais wa Tanzania, Benjamin Mkapa na John Pombe Magufuli.

“Nilipitia kutembelea familia za marafiki zangu wa dhati Marais Benjamin Mkapa na John Magufuli. Ilikuwa furaha yangu kumwona Mama Mkapa na Mama Janeth Magufuli wakiwa wachangamfu. Mungu azilaze roho zao (marais hao wawili) mahali pema peponi,”  Odinga alisema kupitia ujumbe huo.

Marehemu Mkapa aliyehudumu kama Rais wa tatu wa Tanzania alifariki tarehe 24 Julai, 2020 ilhali marehemu Magufuli ambaye alihudumu kama Rais wa tano wa nchi alifariki tarehe 17 Machi, 2021.

error: Content is protected !!