August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Aubameyang azinduka Arsenal ikishusha mvua ya magoli

Spread the love

 

STAA wa Arsenal aliyekuwa na ukame wa magoli, Pierre-Emerick Aubameyang jana tarehe 25 Agosti, 2021 amezinduka na kuifungia timu yake magoli matatu ‘hat-trick’ dhidi West bromwich Albion kwenye mchezo wa raundi ya pili ya kombe la Carabao. Anaripoti Wiston Josia TUDARCo … (endelea).

Katika mchezo huo ambao Arsenal ilishinda goli 6-0, mbali magoli ya Aubameyang, Nicolas Pepe, Bukayo Saka na Alexandre Lacazette kila mmoja alitupia kitu nyavuni.

Mtanange huo uliopigwa katika uwanja wa The Hawthorns umefufua matumaini ya ushindi kwa klabu hiyo kutoka jijini London – England baada ya kuanza vibaya katika msimu mpya wa ligi kuu nchini kwa kuchapwa mechi zote mbili za awali.

Kwa ushindi huo, sasa Kocha Mkuu wa Arsenal Mikel Arteta amerejesha tabasamu na morali kuelekea katika mchezo wa ligi kuu unaotarajiwa kupigwa wikiendi hii kati ya Arsenal na Manchester City.

error: Content is protected !!