Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko THRDC yawapa neno wapinga chanjo ya Korona
Habari Mchanganyiko

THRDC yawapa neno wapinga chanjo ya Korona

Onesmo Olengurumwa, Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC)
Spread the love

 

MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umewaomba Watanzania wasikwamishe mpango wa Serikali, wa kuwachanja wananchi chanjo ya Ugonjwa wa Korona (UVIKO-19). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Wito huo umetolewa leo Jumanne, tarehe 27 Julai 2021 na Mratibu wa Kitaifa wa THRDC, Onesmo Olengurumwa, akizungumza na wanahabari mkoani Dar es Salaam.

Olengurumwa amesema kuwa, Watanzania wanapaswa kuungana na Serikali katika kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa huo, badala ya kufifisha jitihada zake.

“Tunapenda kuwakemea watu wote wanaotaka kufifisha jitihada za Tanzania, kupambana na Korona. Janga la Korona ni la pamoja, tunapaswa kuungana kama Watanzania,” amesema Olengurumwa.

          Soma zaidi:-

Wakati huo huo, Olengurumwa amepongeza hatua ya Serikali ya kuungana na dunia, katika kukabiliana na Korona kwa kutumia chanjo.

“Serikali kuleta chanjo ni jambo jema, ni kutoa fursa kwa Watanzania wanaotaka kuchanjwa. Ni jambo jema kuwaletea na kuwapa bure,” amesema Olengurumwa.

Miongoni mwa watu waliotangaza hadharani msimamo wa kupinga zoezi hilo, ni Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, aliyeishauri Serikali isitoe chanjo hizo kwa wananchi, kwa madai kwamba hazijathibitishwa ubora wake.

Akihubiri katika kanisa lake hilo lililopo Ubungo mkoani Dar es Salaam, Jumapili iliyopita, Askofu Gwajima alidai kwamba, hakuna utafiti wa kisayansi uliofanyika kubaini madhara ya chanjo hizo, kwa mtu anayechanjwa.

Hata hivyo, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, hivi karibuni alisema Serikali imekubali kuingiza chanjo hizo, baada ya kujiridhisha kuwa hazina madhara kiafya.

Tarehe 24 Julai 2021, Serikali ya Tanzania ilipokea dozi 1,058,400 za chanjo ya Korona , kutoka katika Serikali ya Marekani, kupitia mpango wake wa Covax. Unaolenga kusaidia nchi zinazoendelea katika kukabiliana na janga hilo. Chanjo hizo ni aina ya Johnson.

Kesho tarehe 28 Julai 2021, Rais Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuzindua zoezi la ugawaji wa chanjo hizo, Ikulu jijini Dar es Salaam. Ambapo atachanjwa chanjo hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Equity Bank yaendelea kusotea mabilioni ya fedha mahakama rufani

Spread the loveBENKI za Equity ya Tanzania na Kenya, zimeendelea kupambana mahakamani...

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

error: Content is protected !!