June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mjukuu wa Mwalimu Nyerere afariki dunia

Sophia Nyerere

Spread the love

 

SOPHIA Nyerere, ambaye ni mjukuu wa Baba wa Taifa la Tanzania, Hayati Julius Nyerere, amefariki dunia leo Jumanne, tarehe 27 Julai 2021, mkoani Dar es Salaam. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa ya kifo hicho imetolewa leo na familia ya Nyerere, ambayo imesema Sophia amefariki dunia kwenye Hospitali ya Mzena, mkoani Dar es Salaam, alikokuwa anapatiwa matibabu.

Marehemu Sophia alikuwa Mtoto wa Hayati John Nyerere, aliyefariki dunia Mei 2015. John alikuwa mtoto wa nne wa Mwalimu Nyerere.

Taarifa ya familia hiyo imesema, kwa sasa msiba uko nyumbani kwa Mwalimu Nyerere, maeneo ya Mikocheni mkoaniu Dar es Salaam.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, kwa taarifa zaidi kuhusu msiba huo na chanzo cha kifo cha Sophia.

error: Content is protected !!