Sunday , 19 May 2024
Home Kitengo Michezo Kocha Yanga aingia mitini Kigoma, TFF yamtimua Siwa
Michezo

Kocha Yanga aingia mitini Kigoma, TFF yamtimua Siwa

Nasriddine Nabi, Kocha wa Yanga (katikati)
Spread the love

 

KOCHA mkuu wa kikosi cha Yanga, Nasriddine Nabi ameshindwa kutokea kwenye mkutano na wanahabari kuelekea mchezo wa fainali wa kombe la Shirikisho, dhidi ya watani wao Simba. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Kigoma…(endelea).

Mchezo huo, utafanyika kesho Jumapili tarehe 25 Julai 2021, kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma, kuanzia saa 9:30 alasiri.

Katika ratiba ya siku ya leo Jumamosi, iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), ilionyesha kocha wa Yanga alitakiwa kufanya mkutano na wanahabari kwenye moja ya kumbi za Uwanja wa Lake Tanganyika majira ya saa 5 asubuhi, mara baada ya Simba kumaliza saa 4:30.

Wachezaji wa Yanga wakiwasili Kigoma

Kocha huyo alishindwa kutokea pamoja na nahodha wa timu hiyo na badala yake alimtuma kocha wa makipa Razak Siwa katika mkutano huo, ambaye aliondolewa na Afisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo.

Aidha, katika makubaliano yaliyofanyika hapo awali kati ya klabu hizo mbili na TFF, ni kuleta makocha wakuu kwenye mkutano huo pamoja na manahodha na sio mtu mwengine.

Razak Siwa

Katika hatua nyingine, kikosi cha Yanga, majira ya saa 10 kitatembelea Uwanja huo (Pitch visiting), na baada ya hapo kitaelekea kufanya mazoezi yake ya mwisho kwenye uwanja wa Chuo cha Hali ya Hewa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Uingereza, Hispania, Italia na Ufaransa kinawaka leo

Spread the loveLIGI mbalimbali barani ulaya kuendelea leo na michezokadhaa mikali itakwenda...

Michezo

Leo mkwanja upo Meridianbet, usipishane nao

Spread the love  Siku ya leo ni nzuri sana kwa wewe mtumiaji...

Michezo

Anza wikendi yako na Meridianbet, upige mkwanja wa maana

Spread the love Siku ya leo ni nzuri sana kwa wewe mtumiaji...

Habari MchanganyikoMichezo

Arafat atoka bima na kurejea kwenye benki

Spread the loveRais wa Zanzibar Hussein Mwinyi amemteua Arafat Ally Haji kuwa...

error: Content is protected !!