June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Silinde apigwa butwaa, maabara kutokamilika miaka 10

Spread the love

 

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, David Silinde ameshangazwa na kutofautiana kwa taarifa ya ujenzi wa maabara ambayo imechukua takribani miaka kumi pasina kukamilika. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Silinde amekutana na mkanganyiko huo jana Ijumaa tarehe 23 Julai 2021, alipofanya ziara ya ukaguzi katika Shule ya Sekondari Nkome, Mkoa wa Geita

Akiwa shuleni hapo, Silinde aliagiza Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), kufanya ukaguzi wa ujenzi wa maabara tatu wa shule hizo baada ya kubainika gharama iliyotumika ni kubwa na haiendani na majengo ambayo hayajakamilika kwa zaidi ya miaka 10.

Ujenzi wa maabara hizo ni fedha zilizotolewa na GGM, kupitia mpango wa huduma za jamii (CSR).

Katika taarifa iliyosomwa mbele yake ilionekana kutofautina na taarifa iliyotolewa na GGM kuwa maabara hizo zimekamilika kwa gharama ya Sh.86 milioni wakati uhalisia unaonesha maabara hazijakamilika.

Silinde baada ya kukagua alitoa maelezo ya kuandikwa barua ya maelezo ya kina gharama za ujenzi kwenda kwa katibu mkuu Tamisemi na nakala kwa waziri na naibu waziri zifike ndani ya siku saba na ikiibanika kuna mtumishi wa serikali ameshiriki katika ubadhilifu wa fedha basi atarudisha fedha hizo na kuchukuliwa hatu za kisheria.

Kwa upande wake, Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Kasheku ‘Musukuma’ alimweleza Silinde kuwa fedha za CSR kulingana na maelezo ya mgodi wa GGM ni kuwa maabara hizo zimekamilika lakini ukiangalia uhalisia wa jengo hali hailidhishi.

Msukuma aliomba serikali ingilie kati kusaidia umaliziaji wa maabara hizo ili wanafunzi waanze kutumia.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wlaya ya Geita, Edith Mpinzile alimweleza Silinde kuwa walipokea vifaa vyenye thamani ya zaidi Sh.47 milion kutoka GGM na Sh.20 milion ambao walitoa kwenye fedha za makusanyo ya ndani.

error: Content is protected !!