June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waziri Ummy alipia mashabiki 1000 Coastal, wachezaji awaahidi…

Spread the love

 

WAZIRI Ofisi ya Rais-Tamisemi, Ummy Mwalimu amewaahidi Sh.5 milioni, wachezaji wa Coastal Union endapo watafanikiwa kubaki Ligi Kuu Tanzania bara huku akilipia tiketi za mashabiki 1,000. Anaripoti Mwandishi Wetu, Tanga…(endelea).

Coastal Union inashika Uwanja wa Mkwakwani Tanga leo Jumamosi, tarehe 24 Julai 2021, kucheza na Pamba ya jijini Mwanza, kuwania kusalia au kupanda Ligi Kuu.

Katika mchezo wa awali uliochezwa Mwanza, timu hizo zilimaliza dakika 90 kwa kufungana 2-2.

Leo asubuhi, Ummy ambaye ni Mbunge wa Tanga Mjini (CCM), ametembelea kambi ya wachezaji wa Coastal Union ambapo amezungumza nao na kuwaahidi kitita hicho cha fedha ikiwa ni kuwatia moyo.

Kuhusu tiketi hizo za bure, Waziri Ummy amesema, zitapatikana milangoni Mkwakwani na Ofisi ya Mbunge wa Tanga Mjini kuanzia saa 5 asubuhi.

Mchezo mwingine unapigwa Uwanja wa Jamhuri Morogoro kati ya Mtibwa Sugar dhidi Transit Camp.

Katika mchezo wa awali ulipigwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Mtibwa iliibuka na ushindi mnono wa 4-1.

error: Content is protected !!