June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Azam yawatema wanne wakimataifa, yuko Chirwa

Spread the love

 

TIMU ya Azam FC ya Chamanzi Dar es Salaam nchini Tanzania, imetangaza kuachana na wachezaji wake wanne wa kimataifa akiwemo mshambuliaji Obrey Chirwa raia wa Zambia. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Azam imetangaza kuachana na wachezaji hao leo Jumamosi, tarehe 24 Julai 2021 kupitia kurasa zake za kijamii.

“Tumefikia makubaliano ya pande mbili ya kuachana na wachezaji wetu wanne wa kimataifa.”

“Wachezaji hao ni beki wa kati, Yakubu Mohammed, kiungo Ally Niyonzima, mshambuliaji Mpiana Monzinzi na Obrey Chirwa, ambaye mkataba wake umemalizika,” imeeleza Azam na kuongeza

“Azam FC tunawashukuru kwa mchango wao waliotoa katika klabu hii bora kipindi chote walichokuwa nasi na tunawatakia kila la kheri huko waendako.”

error: Content is protected !!