Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Michezo TFF kicheko Mahakamani, zuio la uchaguzi laondolewa
MichezoTangulizi

TFF kicheko Mahakamani, zuio la uchaguzi laondolewa

Walace Karia, Rais wa TFF
Spread the love

 

MAHAKAMA Kuu kanda ya Dar es Salaam, imeiweka pembeni kesi ndogo namba 305, ya zuio la shughuli za uchaguzi TFF, na kutaka kuanza kusikilizwa kwa kesi ya msingi na kutolea maamuzi kabla ya tarehe ya uchaguizi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Uchaguzi huo, utafanyika jijini Tanga, Agosti 7, mwaka huu ambapo mpaka sasa kamati ya uchaguzi imempitisha Walaace karia kuwa mgombea pekee katika nafasi hiyo.

Katika hukumu hiyo ndogo iliyotolewa kwenye shauri hilo, ambalo lipo chini ya Jaji Edwin Kakolaki, Mahakama iliona kwa sasa ijikite kwenye kesi ya msingi kwa madai ya kuwa muda bado upo wa kutosha na kutolea uwamuzi katika wakati sahihi.

Kesi hiyo ambayo ilifunguliwa Mahakamani hapo na mwanamichezo Ally Salehe ‘Alberto’ Julai Mosi Mwaka huu, kwa kudai kuwa uchaguzi huo haukufuata kanuni, hasa kwenye ibara ya 30, ambayo inaonekana kubagua wagombea kutoka Zanzibar.

Akizungumza mara baada ya kesi hiyo kuahilishwa Wakili anayemsimamia Ally Salehe kwenye shauri hilo, Frank Chacha alisema kuwa, Mahakama imeamua kutumia busara kwa kuwa suala hili lipo kwa muundo wa haraka na lisikilizwe kabla ya tarehe ya uchaguzi.

“Mahakama kuu kwa busara zake imeona kwa kuwa suala hili lipo kwa muundo wa haraka, haizui shughuli yoyote kwa sasa na ilichoamua shauri Mama namba 98/2021lisikilizwe haraka.”

“Hapata kuwa na athari kwa sababu kabla ya tarehe 7 kufika uamuzi utakuwa umeshatoka.” Alisema Chacha

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

error: Content is protected !!