Saturday , 10 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge awakutanisha vijana kujadili kero zao
Habari za Siasa

Mbunge awakutanisha vijana kujadili kero zao

Spread the love

 

MBUNGE wa Viti Maalum, Conchesta Rwamlaza amekutana na vijana zaidi ya 300 wa jimbo la Bukoba vijijini lengo ikiwa kusikiliza kero, maoni ya vijana hao ili aweze kuyawasilisha bungeni. Anaripoti Danson Kaijage, Bukoba … (endelea).

Mbali na kusikiliza kero za vijana, tayari ametoa elimu ya kujikinga na virusi vya ugonjwa corona awamu ya tatu pamoja na kuwashonea barakoa.

Akizungumza na vijana hao, leo Ijumaa tarehe 16 Julai 2021, Conchesta amesema, kwa sasa kuna wimbi la ugonjwa wa corona awamu ya tatu na kirusi hicho kwa sasa akichagui kijana au mzee wala mtoto.

Mbunge huyo amesema, kutokana na umuhimu wa kuwepo kwa vijana ni lazima kuhakikisha wanajikinga na kuepukana na mikusanyiko isiyokuwa razima.

Conchesta Rwamlaza

Akizungumza na vijana hao Conchesta amesema vijana wanatakiwa kuhakikisha wanakuwa makini zaidi katika kutunza afya zao.

Pamoja na mambo mengine Conchesta amewataka vijana kuhakikisha wanafanya kazi ili kujikwamua katika umasikini.

“Lazima vijana tujipange katika kufanya kazi na msikubali kukaa kwenye vijiwe bali kuweni wabunifu katika kufanya kazi sambamba na kujihusisha na ujasiliamali,” amesema na kuongeza;

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lussu: Mkataba wa DP bandarini si wa miaka 100

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesema hakuna ukweli wowote...

Habari za SiasaTangulizi

Maulid Mtulia: Kutoka ubunge hadi U-DAS

Spread the love ALIYEKUWA mbunge wa Kinondoni, kupitia vyama vya The Civil...

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

error: Content is protected !!