July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ali Kiba akwaa ubalozi wa kinywaji

Spread the love

 

MSANII wa muziki nchini Tanzania, Ali Kiba amesaini mkataba wa kinywaji cha “Power Horse” kuwa balozi wa kinywaji hicho. Anaripoti Matlida Peter, Dar es Salaam … (endelea).

Mkataba huo, umesainiwa leo Ijumaa, tarehe 16 Julai 2021, jijini Dar es Salaam, ikuhusika pande mbili za Ali Kiba na kampuni ya kinywaji hicho.

Mara baada ya kusaini mkataba huo, Ali Kiba amesema, atatumia nafasi hiyo kukitangaza kinywaji hicho nchi nzima.

Msanii huyo, amewateua Mwijaku, Soudybrown, pamoja Danzak trainer kuwa wahamasishaji wa kinywaji hicho.

Awali, kampuni ya Power Horse imesema, imeamua kumchagua Ali Kiba kuwa balozi wao kutokana na umaarufu wake na ushawishi wake kwenye jamii.

Power Horse wamesema, Ali Kiba atatumia nafasi yake ya usanii kukitangaza vyema kinywaji hicho kisichokuwa na kilevi.

error: Content is protected !!