Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Benki ya Dunia kuipa mabilioni tume ya umwagilijia kanda kaskazini
Habari Mchanganyiko

Benki ya Dunia kuipa mabilioni tume ya umwagilijia kanda kaskazini

Spread the love

 

BENKI ya Dunia (WB), imekubali kuipatia Serikali ya Tanzania, kiasi cha Sh. 108 bilioni, Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Kanda ya Kaskazini. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Fedha hizo, zitatumika kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya umwagilia, katika eneo hilo la Kanda ya Kaskazini.

Hayo yameelezwa jana Jumanne, tarehe 6 Julai 2021 na Mhandisi wa Umwagiliaji mkoani Kilimanjaro, Saidi Ibrahim, wakati wa semina elekezi iliyoandaliwa na Bodi ya Maji Bonde la Pangani.

Semina hiyo, iliwashirikisha wenyeviti wa Jumuiya za watumia maji, makatibu wa mifereji pamoja na wadau mbalimbali wanaojishughulisha na kilimo cha umwagiliaji.

Alisema, benki ya dunia imekubali kuipatia tume ya umwagiliaji mkoa Kilimanjaro, Sh. 58 bilioni na mkoa wa Arusha utapata kiasi cha Sh. 40 bilioni, ambapo fedha zingine zilizobaki zitatumika kwa ajili ya kuendesha mafunzo.

“Kuna fedha sisi kama wataalam wa Tume ya umwagiliaji mkoa Kilimanjaro kwa kushirikiana na Bodi ya Maji Bonde la Pangani, tuliweza kutafuta wafadhili kutoka Benki ya dunia na walitukubalia kutupatia shilingi bilioni 108,” alieleza Mhandisi Ibrahim.

Alisema, kupatikana kwa fedha hizo, kutawezesha kukamilisha miradi 23 ya umwagiliaji iliyopo ndani ya halmashauri saba za mkoa wa Kilimanjaro.

Aidha, katika mwaka wa fedha wa 2021/22 tume ya taifa ya umwagiliaji iliomba miradi mingi kupitia vyanzo vyake vya ndani.

Mkoa wa Kilimanjaro ni miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa kuwa na shughuli za umwagiliaji hususan kwenye vyanzo vizuri vilivyo na maji.

Tume ya umwagiliaji mkoani Kilimanjaro, tayari imeainisha mabonde yote ya maji yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji, kwa lengo la kuhakikisha kuwa maeneo yote ya umwagiliaji yanapanuliwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!