Friday , 3 February 2023
Home Health Covid-19: Uhaba mitungi ya Oxygen washtua watu, Zitto aiamsha Serikali
Health

Covid-19: Uhaba mitungi ya Oxygen washtua watu, Zitto aiamsha Serikali

Spread the love

 

TAARIFA ya upungufu wa mitungi ya kuhifadhia hewa ya Oksijeni ‘Oxygen’, jijini Mwanza,kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wenye matatizo ya upumuaji, ikiwemo ugonjwa wa homa kali ya mapafu, inayosabishwa na Virusi vya Corona (Covid-19), imeshtua watu.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa hizo zilitolewa jana tarehe 6 Julai 2021 na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando, jijini Mwanza, Dk. Fabian Massaga, katika kikao cha wadau wa kupambana na Covid-19, kilichoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel.

Katika kikao hicho, Dk. Massaga alisema kila siku hospitali hiyo inahitaji mitungi ya gesi 300, lakini inayozalishwa ni 100. Na kuomba msaada kutoka kwa wadau ili ipatikane 500 kwa siku, kulingana na mahitaji ya wagonjwa.

Kongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema taarifa hiyo ni sehemu ndogo ya changamoto katika kukabiliana na mlipuko wa Covid-19.

Mwanasiasa huyo amesema kuwa, hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kukabiliana na janga hilo, hazitoshi, huku akiitaka iangalie upya uamuzi wa kuruhusu mikusanyiko ya watu.

“Licha ya hatua mpya na bora kuchukuliwa na Serikali, dhidi ya Covid-19 Tanzania bado hatua hizo hazitoshi. Taarifa ya mitungi ya gesi huko Mwanza ni tone tu, la tatizo kubwa zaidi la Corona nchini,”

Zitto Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo

“Mikusanyiko inaendelea kila mahala , siasa, michezo, biashara na kadhalika, tunaua Watu,” ameandika Zitto katika ukurasa wake wa Twitter.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), mkoani Shinyanga, Emmanuel Ntobi amesema taarifa hizo zinaashiria maambukizi ya Covid-19 yapo na kuwataka Watanzania wachukue tahadhari dhidi ya maambukizi yake.

“Kuwa na upungufu wa mitungi ya oksijeni kwa sasa maana yake Bugando imezidiwa na wagonjwa wa Covid-19, jiongeze, jikinge, uwakingine na wengine Covid-19 ipo,” ameandika Ntobi katika ukurasa wake wa Twitter.

Akizungumza na Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), tarehe 25 Juni 2021, Rais Samia Suluhu Hassan, aliwatahadharisha Watanzania dhidi ya maambukizi ya wimbi la tatu la Covid-19, akiwataka wachukue hatua za kujikinga.

Katika mkutano huo uliofanyika mkoani Dar es Salaam na kurushwa mubashara katika vyombo vya habari, Rais Samia alisema kuna ishara za uwepo wa wagonjwa wa wimbi hilo nchini.

Tangu alipoingia madarakani tarehe 19 Machi 2021, kufuatia kifo cha mtangulizi wake, Hayati John Magufuli, Rais Samia amechukua hatua mbalimbali katika kukabiliana na Covid-19.

Miongoni mwa hatua hizo ni kuunda timu ya wataalamu kwa ajili ya kuchunguza mwenendo wa Covid-19 nchini. Ambayo ilitoa mapendekezo yake juu ya namna ya kukabiliana na janga hilo.

Pia, Serikali ya Rais Samia imeandaa muongozo wa uingizwaji na utoaji chanjo ya ugonjwa huo, ambao uko mbioni kuanza kazi.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Hali kadhalika, Serikali ya Rais Samia, imetoa muongozo wa namna ya kudhibiti maambukizi ya Covid-19, shuleni, vyuoni na kwenye taasisi za elimu, na kwamba taasisi hizo zimeelekezwa kuweka mazingira ya wanafunzi kunawa mikono na kuvaa barakoa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Health

Wananchi Same wahamasishwa kuchangia damu kwa hiari

Spread the loveHOSPITALI ya Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro imetoa elimu ya ...

Health

Decision to Leave Is This Century’s First Great Erotic Thriller

Spread the loveMauris mattis auctor cursus. Phasellus tellus tellus, imperdiet ut imperdiet...

Health

Winners of Wildlife Photographer of the Year 2022

Spread the loveMauris mattis auctor cursus. Phasellus tellus tellus, imperdiet ut imperdiet...

Health

Technology Can Make Your Relationships Shallower

Spread the loveMauris mattis auctor cursus. Phasellus tellus tellus, imperdiet ut imperdiet...

error: Content is protected !!