July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwanakijiji Morogoro ajishindia gari la milioni 169 kutoka NMB

Spread the love

 

MKAZI wa Kijiji cha Kinole, Mkoa wa Morogoro nchini Tanzania, Abdallah Mohammed, amejishindia gari jipya aina ya Toyota Fortuner yenye thamani ya Sh.169 milioni kutoka promosheni ya Benki ya NMB ya “Bonge la Mpango.” Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Gari hiyo, imekabidhiwa leo Jumanne, tarehe 7 Julai 2021 na Kaimu Afisa Mkuu Ukaguzi wa ndani wa Benki ya NMB, Benedicto Baragomwa, shughuli iliyofanyikia
Soko Kuu la Kingalu karibu na tawi la NMB la Wami- Morogoro.

Baragomwa, amesema, zawadi zilizonyakuliwa katika promosheni hiyo ni pamoja na fedha taslimu walizoshinda wateja 120. Nyingine ni pikipiki za miguu mitatu ‘bajaji’ 24 aina ya LIFAN na Kirikuu tatu za muundo wa TATA Ace.

Amesema, promosheni hiyo, ilifanya uwekezaji huo kwa ajili ya kutambua mchango wa wateja katika mafanikio yake ikiwemo kuandika historia katika tasnia ya kibenki kwa kupata faida kubwa kuwahi kutengenezwa na benki nchini ya Sh.206 bilioni mwaka 2020.

7

“Mwezi Februari tulizindua kampeni maalumu yenye makusudi ya kurejesha faida kwa wateja pamoja na kuhamasisha utamaduni wa kujiwekea akiba kwa Watanzania,” amesema Baragomwa

“Leo ndo tumefikia kilele cha Bonge la Mpango…Kampeni hii ya miezi mitatu ililenga kuwahamasisha wasio na akaunti ya benki nchini kuja kufungua na kutunza akiba zao kwa njia salama zaidi na Benki ya NMB,” amesema

Naye mshindi wa gari hilo, Mohammed mwenye miaka 50 amesema “hatimaye nimeamini kabisa mimi ndiye kweli mshindi wa zawadi kubwa ya shindano hili ingawa nilipata taarifa ya ushindi wangu katikati ya mwezi jana.”

Mohammed ambaye ni mfanyabiashara akiwa na watoto watano amesema, mpaka anakbidhiwa rasmi zawadi hiyo, aliuchukulia ushindi wake kama ndoto, kutokana na sababu kadhaa.

Amezitaja sababu hizo ni; “mimi kuishinda hii zawadi kubwa kama ndoto za alinacha. Pamoja na kuwa mteja mwaminifu wa NMB, kwanza mimi ni mwanakijiji harafu mfanyabiashara mdogo tu wakati benki hii ina zaidi ya wateja zaidi ya milioni nne wakiwemo matajiri wakubwa.”

“Ushindi wangu umenifunza jambo jingine kubwa kuhusu NMB. Kumbe ni benki ya kila Mtanzania bila kujali hadhi yake katika jamii na kiuchumi. Sizingekuwepo huduma za kibenki za kimtandao wala nisingekuwa hata mteja wake acha kuinyakua hii zawadi,” amesema Abdallah

error: Content is protected !!