Wednesday , 8 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge CCM: Serikali imeingizwa mkenge
Habari za Siasa

Mbunge CCM: Serikali imeingizwa mkenge

Jerry Slaa, Mbunge wa Ukonga
Spread the love

 

JERRY Slaa, Mbunge wa Ukonga, jijini Dar es Salaam (CCM), amesema serikali imeingizwa mkenge katika pendekezo lake la kufuta adhabu ya asilimia 100, kwa kampuni zinazoshindwa kutekeleza matakwa ya kanuni za ukokotoaji wa kodi za kimataifa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mbunge huyo alitoa kauli hiyo jana Jumatano, tarehe 23 Juni 2021, wakati akichangia mjadala wa Muswada wa Sheria ya Fedha ya 2021/22, bungeni jijini Dodoma, uliowasilishwa bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba.

Alidai, kampuni nyingi za kimataifa hutumia kanuni hizo kupunja mapato ya serikali kwa udanganyifu, kwa kutaja kiwango kidogo cha mapato yao ikilinganishwa na mapato halali inazopata.

Mwanasiasa huyo amesema, kaguzi za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), zinaonesha asilimia 33 ya kampuni zimeanishwa kuwa hatari kupitiua kanuni hizo.

“Ukisoma bajeti ukurasa wa 52 kuna maneno ya kufanya marekebisho kwenye regulation za transfer price regulation za 2014, kuondoa adhabu ya asilimia 100 kwa watakaobainika kufanya vitendo hivi vya transfer prices,” amesema Slaa.

Slaa ameongeza “katika mambo makubwa yanayopoteza kodi ya nchi yetu, hasa kwenye kampuni kubwa ni ya transfer price, ukaguzi wa CAG unaonesha asilimia 33 ya makampuni yameanishwa kuwa hatari katika transfer price.”

Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango

Mbunge huyo amesema, kama Serikali itatekeleza pendekezo la kufuta adhabu hiyo, Taifa litaingia hasara kwa kuwa kampuni za kimataifa zitakuwa zinatumia sheria hiyo, kuipunja mapato Serikali, kwa njia za udanganyifu.

“Niliombe Bunge hili na waziri wa fedha kwa lugha ya mjini tunasema, hii imechomekewa. Usisaini kanuni hii, ukisaini kanuni hii unaenda kuitia Serikali hasara kubwa ambayo huko nyuma tulikuwa tumeondoka,” amesema Slaa.

Mbunge huyo wa Ukonga amesema, hatua hiyo inarudisha nyuma jitihada za Serikali kuiongozea nguvu Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), katika ukusanyaji mapato kupitia Kitengo cha Ushuru cha Kimataifa (ITU), za kudhibiti utoroshwaji wa fedha nchini kupitia sheria hiyo.

“CAG ametoa mapendekezo kwa wizara kuisapoti TRA, kuongeza nguvu kwenye suala la kusimamia kitengo ITU, katika kuhakikisha tunaondosha utoroshaji wa fedha nchini, kupitia transfer price,”

“Kwa bahati mbaya sana, wizara ya fedha badala ya kutengeneza utaratibu kutoa sapoti inaleta mabadiliko ya kwenda kuondoa adhabu kwenye jambo ambalo ni kosa kisheria,” amesema Slaa.

Katika mapendekezo ya bajeti kuu ya Serikali, kwa mwaka wa fedha 2021/22, iliyowasilishwa bungeni jijini Dodoma na Dk. Mwigulu, tarehe 10 Juni 2021, Serikali ilipanga kufuta kifungu hicho, ili kuwaondolea walipa kodi adhabu kubwa na kuvutia wawekezaji.

Slaa amepinga sababu hiyo, akisema hiyo ni adhabu na wala si kodi “Unaenda kuondosha adhabu, maana yake unaenda kuhalalisha kosa, unaenda kumfanya mtu afanye kosa kwa amani kwamba anajua hakuna adhabu.

“Nilitegemea adhabu hii itoke asilimia 100 iende zaidi ya hapo, ili kutengeneza woga kwa kampuni kubwa ambazo kwa miaka mingi wanalipa kodi ndogo kuliko wafanyabaishara wadogo,” alisema Slaa na kuongeza:

“Mnaposema mnataka kufuta kanuni hii ya adhabu kwa kigezo cha kusema eti unahamasisha uwekezaji aliendaika hii Mungu anamuona, ameandika akijua wazi haendi kukuza uwekezaji.”

Hata hivyo, pendekezo hilo la kufutwa adhabu hilo halikuwemo katika Muswada wa Sheria ya Fedha, uliowasilishwa bungeni jana na Dk. Mwilgulu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mpina mwiba CCM, ahofia kuzibwa mdomo

Spread the loveWAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM), kikijinasibu kuwa kinara wa demokrasia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mabeyo ametuepusha

Spread the loveNIMEGUSWA na uadilifu, utiifu na uaminifu wa Mkuu mstaafu wa...

Habari za SiasaTangulizi

CCM yaitaka TAKUKURU kuichunguza Chadema tuhuma alizoibua Lissu

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana...

error: Content is protected !!