July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

RC Makalla ataka barakoa kuvaliwa Dar

Spread the love

 

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), Amos Makalla, amewataka wananchi mkoani humo kuchukua tahadhari ya maambukuzi ya corona (COVID-19), kwa kuvaa barakoa kwa usahihi wawapo kwenye mikusanyiko, vyombo vya usafiri, masoko, sherehe, maofisini na vituo vya Afya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

RC Makalla ametoa maagizo hayo leo Alhamisi, tarehe 24 Juni 2021, wakati akizungumza na wakuu wa wilaya, wakuu wa taasisi za umma na za kiraia na vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha wanasimamia ipasavyo maelekezo hayo.

Makalla amesisitiza wananchi, kunawa mikono kwa maji tiririka kwa sabuni mara kwa mara.

 

“Wananchi kuwahi mapema vituo vya afya wanapobaini dalili za corona ikiwemo homa kali, mafua makali, kikohozi, uchovu na nyingine. Pia, kufanya mazoezi ili kuimarisha kinga ya mwili,” amesema Makalla

Mkuu huyo wa mkoa amewataka wananchi, kula mlo kamili na kutoa uangalizi mzuri kwa watu walio kwenye hatari ya kupata madhara wakiwemo wazee na wenye magonjwa sugu.

error: Content is protected !!