August 4, 2021

Uhuru hauna Mipaka

TFF yamtoa kifungoni Mwakalebela

Frederick Mwakalebela, Makamu Mwenyekiti wa Yanga

Spread the love

 

Kamati ya maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imemuondoa kifungoni Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Fedrick Mwakalebela, mara baada ya kukili kosa mbele ya kamati hiyo na kutaka kuondolewa kwenye adhabu hiyo ambayo alishaanza kuitumikia. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Kamati hiyo ilimfungia kiongozi huyo, kujihusisha na soka katika kipindi cha miaka miatno na kulipa faini ya Shilingi 7,000,000 milioni mara baada ya kuvishutumu vyombo vianavyo simamia Ligi kuu kuwa inaihujumu Yanga.

Taarifa yakuondolewa kwenye adhabu hiyo, iliyotolewa na Tff ilieleza kuwa, Makamu Mwenyekiti huyo wa Yanga alipeleka maombi ya kuondolewa kwenye kifungo hiyo mbele ya kamati hiyo, na kukili kufanya kosa na kutaka kupewa tena nafasi ya kuutumikia mpira kwa kuzingatia sharia na kanuni zilizopo.

Katika kikao chake cha tarehe 23 Juni 2021, kamati hiyo ilisikiliza maombi hayo ya Mwakalebela na kukubaliana na sababu alizozitoa na kumuondolea adhabu hiyo.

Kiongozi huyo alifungiwa Tarehe 2 Aprili, mwaka huu, mara baada ya kulalamikiwa kuwa tarehe 19 Februari 2021,kuitisha mkutano na waandishi wa Habari na kudai kuwa TFF, Bodi ya Ligi na kamati ya uendeshaji na usimamizi wa Ligi, inahujumu klabu ya Yanga madai ambayo alishindwa kuthibitisha mbele ya kamati.

Adhabu ya kumfungia kwa miaka mitano Mwakalebela, ilitolewa kwa kuzingatia kifungu cha 73(4) cha kanuni za maadili ya TFF toleo la 2013.

error: Content is protected !!