Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Michezo Mzanzibari kuwania urais TFF
MichezoTangulizi

Mzanzibari kuwania urais TFF

Ally Saleh 'Alberto'
Spread the love

 

MWANASOKA maarufu nchini, Ally Salehe ‘Alberto,’ amejitosa katika mbio za kuwania urais ndani ya shirikisho la soka nchini (TFF). Anaripoti Saed Kubenea ….(endelea).

Uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo – Tanzania Football Federation – umepangwa kufanyika tarehe 7 Agosti mwaka huu, jijini Tanga.

Akizungumza na MwanaHALISI Online, mwanamichezo huyo amesema, ameamua kujitosa katika kinyang’anyiro hicho, ili kuendeleza mchezo wa soka nchini na kusaidia Zanzibar, kupata uanachama wake katika mashirikisho ya Soka ya CAF na FIFA.

Amesema, “ninakwenda kuendesha na kuendeleza mchezo wa soka. Ninakwenda TFF kusimamia mchezo wa soka, ambao ni kipenzi cha wengi. Ninakwenda TFF, ili kukuza vipaji na kusaidia timu ya taifa, Taifa Stars ifanye vizuri kwenye michuano ya kimataifa.”

Kujitosa kwa Ally Salehe ambaye kitaaluma ni mwanasheria, mwandishi wa habari za michezo na aliyewahi kuwa mtangazaji wa shirika la utangazaji la Uingereza (BBC) na wakala wa kimataifa wa wachezaji wa soka anayetambuliwa na FIFA na CAF, kunatajwa na wachambuzi wa soka, kuwa kumechochea ndimu kwenye uchaguzi huo.

 

Kwa takribani miaka 40 sasa, Zanzibar imekuwa ikililia uanachama wake FIFA na CAF. Miaka 10 iliyopita, wakati wa uongozi wa Ledga Tenga na baadaye Jamal Malinzi, ndipo Zanzibar ilifanikiwa kuwa mwanachama wa muda wa CAF.

Kwa mujibu wa Ally Salehe mwenyewe, amepanga kesho Ijumaa, kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo na Jumamosi mchana anaweza kurejesha, akiwa tayari ametimiza masharti yote yanayotakiwa.

Mpaka sasa, ni wagombea wawili pekee, waliojitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya urais ndani ya TFF. Wagombea hao, ni Wallace Karia, rais anayetetea nafasi yake na Oscar Oscar, ambaye ni mfanyakazi wa kituo cha radio cha E-FM, jijini Dar es Salaam.

Ikiwa mwanasoka huyo mahiri nchini, atajitosa kuwania nafasi hiyo, basi hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Mzanzibari, kugombea nafasi ya urais wa TFF.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Michezo

Jumamosi ya leo ni ya pesa tu kutoka Meridianbet

Spread the love  IKIWA leo hii ni Jumamosi nyingine na tulivu kabisa,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

error: Content is protected !!