May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Djuma Shabani kimeeleweka Yanga

Spread the love

 

Ni kama Yanga sasa wameonekana kufanikiwa kumyakuwa beki wa pembeni kutoka klabu ya AS Vita ya nchini Congo Dr, mara baada ya mjumbe wakamati ya mashindano wa klabu hiyo, Mhandisi Hersi Said kuonekana nchini Congo kukamilisha uhamisho huo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Yanga ambao wiki iliyopita waliripotiwa kumalizana na mchezaji huyo, ambaye amemaliza mkataba wake ndani ya AS Vita, na kuonesha kiwango bora kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Kupitia ukurasa wa kijamii wa Mhandisi Hersi Said ambaye pia ni mkurugezni wa uwekezaji wa kampuni ya Gsm, ambao ni wadhamini wa klabu ya Yanga, alionekana kwenye picha akiwa na Waziri wa Michezo wa nchini Congo, na kuandika kuwa.

Usajili huo utakuwa wa kwanza ndani ya klabu ya Yanga kuelekea msimu ujao wa mashindano ambapo watawakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa mara baada ya Tanzania kufanikiwa kuingiza timu nne.

error: Content is protected !!