Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Mwigulu abainisha mkakati kupunguza foleni Dar, barabara mikoani
Habari za Siasa

Dk. Mwigulu abainisha mkakati kupunguza foleni Dar, barabara mikoani

Spread the love

 

WAZIRI wa Fedha na Mipango nchini Tanzania, Dk. Mwigulu Nchemba, amebainisha mikakati mbalimbali ya kupunguza msongamano jijini Dar es Salaam ni ukarabati wa barabara kilomita 138.5. Anaripoti Nasra Bakari, DMC … (endelea).

Dk. Mwigulu, amesema hayo leo Alhamisi, tarehe 10 Juni 2021, wakati akiwasilisha bungeni jijini Dodoma, taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022.

Amesema, Serikali itaendelea na ujenzi na ukarabati wa barabara za kupunguza msongamano za Jijini Dar es Salaam (km 138.5).

“…pamoja na barabara za mikoa, kuboresha miundombinu ya mabasi yaendayo haraka kwa awamu zote nne, ujenzi wa barabara za juu (Flyover) jijini Dar es Salaam,” amesema Dk. Mwigulu.

Pia, amesema, uboreshaji wa barabara za mzunguko katika Jiji la Dodoma pamoja na barabara za vijijini na mijini kupitia Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura).

“Vilevile, Serikali itaendelea na ujenzi wa madaraja makubwa yakiwemo madaraja ya New Wami (Pwani), Kitengule (Kagera), Kirumi (Mara) na Mkenda (Ruvuma),” amesema

Waziri huyo amesema, kipaumbele kitawekwa katika barabara za lami, zinazofungua fursa za kiuchumi ambazo ni: barabara za Kidatu – Ifakara – Lupilo – Malinyi – Londo – Lumecha/Songea (km 499); Lukuyufusi – Mkenda (km 122.5); Ifakara – Kihansi – Mlimba – Madeke – Kibena (km 220); Tabora – Ipole – Koga – Mpanda (km 365.36) na barabara ya Makutano – Natta – Mugumu/Loliondo – Mto wa Mbu (km 235);

Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango

Zingine ni; Manyoni – Itigi – Tabora (km 259.75); Handeni– Kiberashi – Kijungu – Kibaya – Njoro – Olboloti – Mrijo Chini – Dalai – Bicha – Chambalo – Chemba – Kwa Mtoro – Singida (Km 460); Dodoma – Mtera – Iringa (km 273.3); Dodoma – Babati (km 243.8); Mbeya – Chunya – Makongolosi – Rungwa – Itigi – Mkiwa (km 528) na Kigoma – Kidahwe – Uvinza – Kaliua – Tabora (km 389.7);

Pia, barabara ya Mtwara – Newala – Masasi (km 210); Barabara ya Masasi – Songea – Mbamba Bay (km 343.2); Barabara ya Nzega – Tabora (km 289.7); Barabara ya Msimba – Ruaha Mbuyuni/Ikokoto Mafinga (km 234.8); Igawa – Songwe –Tunduma na Mchepuo wa Mbeya (km 273.5); na Makambako – Songea na Mchepuo wa Songea (km 295).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!