Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari Sakata la rushwa Yanga dhidi ya Prisons latua Bungeni
HabariMichezoTangulizi

Sakata la rushwa Yanga dhidi ya Prisons latua Bungeni

Spread the love

NAIBU waziri wa utumishi na utawala bora Deogratius Ndenjembi amesema kuwa kuna baadhi ya viongozi wa timu mbalimbali hapa nchini wakifungwa na Yanga hasa kihalali hutoa kauli ya kwamba wamehongwa. Anaripoti Kelvin Mwaipungu.

Kauli hiyo ameitoa leo tarehe 4 Mei 2021 Bungeni wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kinondoni Abbas Tarimba.

Katika swali hilo la nyongeza Tarimba kwa Wizara hiyo Tarimba aliuliza kuwa kwenye mchezo wa Yanga dhidi ya Prisons uliofanyika kwenye Uwanja wa Nelson Mandela Sumbawanga kuna mchezaji wa Prisons alitoa tuhuma za Yanga kutaka kuwaonga shilingi 40 milioni.

Wakati akijibu swali hilo Mheshimiwa Ndenjembi alisema kuwa ifike wakati viongozi wa timu hizo wakubali matokeo hasa wanapofungwa kihalali.

Deogratius Ndechembi, Naibu Waziri wa Utumishi na utawala bora

“Kumekuwa kuna tabia ya viongozi wa timu mbalimbali hapa nchini hasa wakifungwa na Yanga kihalali hutoa kauli kwamba wamehongwa, ifike wakati viongozi wa timu hizi wakubali Yanga ndiyo timu bingwa na bora hapa Afrika kwa hiyo wanapofungwa wakubaliane na matokeo”, alisema Naibu Waziri huyo

Akitilia mkazo kwenye jibu la swali hilo Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Inocent Bashungwa alisema kuwa Serikali inashilikiana na vyombo vya usala kuhakikisha wanapambana na rushwa kwa nguvu zote na kuweka mazingira wezeshi ya michezo kukua bila rushwa.

https://www.youtube.com/watch?v=4sfGFemRZDY

“Ningependa kuwapa uhakika waheshima wabunge na watanzania kuwa Serikali hii haitafumbia macho timu au mshilika yoyote kwenye michezo aatakayetumia rushwa ili aweze kujipatia ushindi” alisema Bashungwa

Sakata hilo limeibuka kufuatia Nahodha wa Tanzania Prisons Benjamin Asukile kutoa tuhuma hizo kwa Yanga kutaka kuwaonga kiasi cha shilingi milioni 40 ili waweze kushinda mchezo huo wa hatua ya 16 bora ya michuano ya kombe la Shirikisho.

Asukile aliyasema hayo kwenye mahojiano yake na Azam TV mara baada ya mchezo huo kuisha ambapo Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0, lililofungwa Yacouba Sogne na kuitupa nje Prisons kwenye michuano hiyo.

Abbas Tarimba, Mbunge wa Kinondoni (CCM)

Kufuatia tuhuma hizo uongozi wa klabu ya Yanga kupitia Afisa Habari wao Hassani Bumbulia alisema kuwa wanamtaka mchezaji huyo athibitishe tuhuma hizo mbele ya vyombo husika kwa kuwa amichafua klabu hiyo.

“Hakuna namna Yanga tunaweza kuvumiliwa kuchafuliwa kwa kiwango hiki, tunataka athibitishe hizi tuhuma kivipi na kwa namna gani” alisema Bumbuli

 

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

error: Content is protected !!