Sunday , 19 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia atangaza ajira mpya 40,000
Habari za Siasa

Rais Samia atangaza ajira mpya 40,000

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, ametangaza ajira mpya 40,000 na kupandisha vyeo watumishi 90,000 katika mwaka wa fedha 2021/22. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ajira hizo, zimetangazwa leo Jumamosi na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, katika hotuba yake kwa wafanyakazi ya siku ya Mei Mosi, ambayo imefanyika, Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Amesema, ajira hizo zitakuwa zaidi za kada ya afya na elimu “ili kuwapunguzia watumishi waliopo mzigo” na itagharimu Sh.239 bilioni.

Pia, amesema katika mwaka huo wa fedha 2021/22, watumishi kati ya 85,000 hadi 90,000 watapandishwa vyeo na wataigharimu serikali Sh.449 bilioni “na tutalipa malimbikizo ya mishahara Sh.60 bilioni”

Rais Samia amesema, mabadiliko ya muundo wa utumishi yataigharimu Serikali Sh.120 bilioni.

Amesema, kutokana na hatua hiyo na janga la corona lililotokea mwaka jana, limesababisha kutopandishwa kwa mishahara mwaka huu hadi mwakani.

1 Comment

  • MIMI NAOMBA KUULIZA AJIRA AMBAZO ZILI TANGANZWA NI ELFU 40, LAKN ZILIZOTANGANZWA HATA HAZIFIKI 20ELF , JE//???? KUNA AJIRA ZINGNE TOFAUT NA ZILIZOTANGAZWA???

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RUWASA yachongewa, yateketeza mamilioni kwa maji yenye magadi

Spread the loveSAKATA la ukosefu wa maji wilayani Momba mkoani Songwe limezidi...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Lissu akabidhiwa gari lake, aomba msaada wa matengenezo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu leo Ijumaa amekabidhiwa...

error: Content is protected !!