Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Bila kusafiri hupati Paspoti – Uhamiaji
Habari MchanganyikoTangulizi

Bila kusafiri hupati Paspoti – Uhamiaji

Spread the love

IDARA ya Uhamiaji nchini Tanzania imeeleza, ili mtu yeyote aweze kupewa hati ya kusafiria (paspoti), ni lazima awe na kusudio la kusafiri. Anaandika Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo Jumanne tarehe 16 Machi 2021 na Paul Mselle, Msemaji wa Idara ya Uhamiaji alipozungumza na chombo kimoja cha habari nchini.

Amesema, hati ya kusafiria ni tofauti na vitambulisho vingine vya kawaida, na kwamba hati hiyo ni mali ya serikali.

“…ni lazima awe na dhumuni la kusafiri, kama hana safari hatuwezi kumapatia pasi hiyo,” amesisitiza Mselle.

Ofisa huyo amesema, ni marufuku kwa mtu yeyote kutumia hati hiyo kwa nia ovu, na kwamba kwa kuwa ni mali ya serikali, ikitumika vibaya muhusika anaweza kupokwa.

1 Comment

  • Siku hizi ukitaka kununua tiketi ya ndege unaulizwa namba ya pasipoti, Halikadhalika ukiomba visa au nafasi ya masomo.. Je wakuu wa uhamiaji wanaelewa hilo?
    Ajabu wao wanasema kwanza fanya maandalizi ya safari kisha omba pasipoti

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu wa GGML

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) pamoja na Wakala...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yashiriki maadhimisho Mei Mosi Arusha

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na maelfu ya...

Habari Mchanganyiko

Makonda autaka mgodi kubadilisha maisha ya wana-Geita

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ametoa wito kwa...

Habari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Je, miji ya Uingereza inafilisika?

Spread the loveMNAMO 1890, mwandishi mmoja wa habari Mmarekani aitwaye Julian Ralph...

error: Content is protected !!