May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wenye viwanda Tanzania, NEMC wapewa maagizo

Mwita Waitara, Naibu wa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, amewaagiza wenye viwanda nchini humo, kuajiri wataalamu wa mazingira ili kukidhi matakwa ya kisheria. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Agizo hilo, lilitolewa jana Jumatatu tarehe 15 Machi 2021, na Mwita Waitara, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira, wakati wa ziara yake kikazi katika viwanda vya Sunda, Kiluwa, Fuxing Ltd vya Mlandizi na Kebs cha Kibaha wilayani Kibaha mkoani Pwani kwa lengo la kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2094.

Pamoja na kuwapongeza wawekezaji hao, Waitara aliwataka kufuata sheria na kusisitiza Serikali haitafunga kiwanda na badala yake, itawaelimisha ili waweze kuendana na matakwa ya sheria.

Aidha, Waitara alitoa maelekzo kwa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), kufanya ukaguzi wa uzingatiaji wa hifadhi ya mazingira katika viwanda vyote vya wilaya hiyo na kuandaa ripoti ili Serikali itoe uamuzi, lengo likiwa ni kulinda wananchi wasipate madhara kutokana na baadhi ya viwanda hivyo kubainika vinachafua mazingira.

error: Content is protected !!