May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bila kusafiri hupati Paspoti – Uhamiaji

Spread the love

IDARA ya Uhamiaji nchini Tanzania imeeleza, ili mtu yeyote aweze kupewa hati ya kusafiria (paspoti), ni lazima awe na kusudio la kusafiri. Anaandika Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo Jumanne tarehe 16 Machi 2021 na Paul Mselle, Msemaji wa Idara ya Uhamiaji alipozungumza na chombo kimoja cha habari nchini.

Amesema, hati ya kusafiria ni tofauti na vitambulisho vingine vya kawaida, na kwamba hati hiyo ni mali ya serikali.

“…ni lazima awe na dhumuni la kusafiri, kama hana safari hatuwezi kumapatia pasi hiyo,” amesisitiza Mselle.

Ofisa huyo amesema, ni marufuku kwa mtu yeyote kutumia hati hiyo kwa nia ovu, na kwamba kwa kuwa ni mali ya serikali, ikitumika vibaya muhusika anaweza kupokwa.

error: Content is protected !!