Tuesday , 30 April 2024
Home Kitengo Michezo Simba yaipeleka Al Merreikh CAF
Michezo

Simba yaipeleka Al Merreikh CAF

Barbara Gonzalez, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba
Spread the love

 

UONGOZI wa klabu ya Simba umtaka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kufanya uchunguzi kuhusu klabu ya Al Merreikh kuchezesha wachezaji wawili kwenye mchezo dhidi yao, ambao wamefungiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Sudan. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Al Merreikh waliwavaa Simba kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliofanyika nchini Sudan siku ya Jumamosi tarehe 6 Machi 2021 na kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

Wachezaji ambao klabu ya Simba wanataka wafanyiwe uchunguzi ni Ramadan Ajab na Bakhiet Khamis ambao wanadai kufungiwa miezi sita kutokana na kila mmoja kusaini mikataba na timu mbili.

Taarifa kutoka ndani ya Simba inaeleza kuwa adhabu za wachezaji hao zilianza kuanzia tarehe 21 Januari 2021.

Simba na Al Merreikh wapo kwenye Kundi A ya Ligi Mabingwa Afrika ambapo mpaka sasa Simba ndiyo kinara wa kundi hilo akiwa na pointi saba, akifuatiwa na AS Vita wenye pointi nne, huku nafasi ya tatu ikishikwa na mabingwa watetezi Al Ahly wakiwa na pointi na Al Merreikh wakishika mkia.

Kama CAF wakijilidhisha na madai hayo kwa wachezaji hao kutumika basi Al Merreikh itaondolewa kwenye michuano hiyo kama kanuni ya saba ya mashindano ya CAF inavyoeleza na Simba kupewa pointi tatu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Beti na Meridianbet mechi za leo

Spread the love IKIWA leo hii ni Jumapili tulivu kabisa, Meridianbet wanamkwambia...

Michezo

Jumamosi ya leo ni ya pesa tu kutoka Meridianbet

Spread the love  IKIWA leo hii ni Jumamosi nyingine na tulivu kabisa,...

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

error: Content is protected !!