May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CAF yafuta michuano ya Afcon U-17

Spread the love

 

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limefuta michuano ya kombe la mataifa Afrika chini ya miaka 17 (AfconU17), iliyokuwa ianze tarehe 13-31 Machi 2021, nchini Morocco. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

CAF imetolea uamuzi huo jana Jumatatu tarehe 8 Machi 2021, kupitia kamati yake ya dharura ya michuano hiyo na sababu kuu ikiwa ni ugonjwa unaosababishwa na maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19) na masharti ya Kimataifa ya kusafiri.

Shirikisho hilo, limefuta michuano hiyo hadi hapo baadaye itakapotangazwa tena.

Uamuzi huo, umechukuliwa ikiwa tayari baadhi ya timu zinazoshiriki muchuano hiyo kama za Tanzania na Uganda, zimekwisha wasili nchini Morocco kwa maandalizi.

error: Content is protected !!