Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Michezo Kocha mpya Simba awapandisha mizuka wachezaji
Michezo

Kocha mpya Simba awapandisha mizuka wachezaji

Mohammed Hussein, Nahodha msaidizi wa Simba
Spread the love

 

NAHODHA msaidizi wa klabu ya Simba, Mohammed Hussein amesema kuwa ujio wa kocha wao mpya umeongeza mzuka kwa wachezaji katika kutimiza malengo ya klabu hiyo kwa msimu wa 2020/21. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Kocha huyo ambaye ni raia wa Ufaransa amekuja kuchukua nafasi iliachwa wazi na Sven Vandebroeck aliyetimukia nchini Morocco alitambulishwa na uongozi huo terehe 25 Januari 2021, kwa mkataba wa miaka miwili.

Mohammed Hussein ameyasema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya TP Mazembe kwenye Simba Super Cup na kusema kuwa watahakikisha wanamsaidia kocha huyo kutimiza malengo ya klabu.

“Mwalimu wetu tumempokea ni mpya kwa sababu sisi tupo kwenye na vitu tutakavyo msaidia ni kuhakikisha kwamba tunafikia malengo ya klabu wala haijalishi kaja muda gani.

“Akija kocha mpya mara ya kwanza lazima anaongeza molari licha ya kwamba ilikuwepo na kwa muda mfupi kuna vitu muhimu ametueleza kuhusu umuhimu wa michuano ya kimataifa,” alisema nahodha huyo.

Simba kwa sasa inayoshiriki michuano ya Super Cup ambayo atacheza michezo miwili watakayotumia kama maandalizi kuelekea michuano ya Ligi ya mabingwa ambayo wapo hatua ya makundi na mchezo wa kwanza watacheza tarehe 12 Februari 2021, nchini Congo DR dhidi ya AS Vita.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Jumamosi ya leo ni ya pesa tu kutoka Meridianbet

Spread the love  IKIWA leo hii ni Jumamosi nyingine na tulivu kabisa,...

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

error: Content is protected !!