Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Matiko, Bulaya waitwa CCM
Habari za Siasa

Matiko, Bulaya waitwa CCM

Spread the love

MLANGO wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), umefunguliwa kwa Ester Matiko, Ester Bulaya, Halima Mdee na wengine waliofukuzwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kujiunga. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Wito wa wanasiasa hao waliokuwa wanachama wa Chadema kujiunga na CCM, umetolewa na Dk. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa CCM tarehe 29 Novemba 2020 wakati wakati akifungua semina ya wajumbe wa sekretarieti ya taifa ya halmashauri kuu na kamati ya utekelezaji wa jumuiya za chama hicho.

“Tunawakaribisha.., milango iko wazi” amesema Dk. Bashiru huku akisisitiza “chama cha siasa kinachogharamiwa na watu wa nje, hicho sio chama.”

Dk. Bashiru ametoa kauli hiyo ikiwa ni baada ya Bulaya na wenzake kutimuliwa uanachama wa Chadema kutokana na kukiuka misingi ya chama hicho, kwa kwenda kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalumu.

 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, Dk. Bashiru Ally

Chadema kupitia John Mnyika, katibu mkuu wa chama hicho alipokutana na waandishi wa habari wiki iliyopita alieleza, wanachama  hao 19 walioapishwa kuwa wabunge, walijiteua wenyewe baada ya kuasi msimamo wa Chadema wa kutotambua matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020.

Mbali na Matiko, Bulaya na Mdee kufukuzwa Chadema, wengine ni Katibu Mkuu wa Bavicha, Nusrat Hanje; Katibu Mkuu Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Grace Tendega; Makamu Mwenyekiti Bawacha (Bara), Hawa Mwaifunga; Naibu Katibu Mkuu Bawacha, Jesca Kishoa na Katibu Mwenezi Bawacha, Agnesta Lambat.

Yupo pia Mwenyekiti wa Chadema Mkoa Mtwara, Tunza Malapo, Ceciia Pareso, Asia Mwadin Mohamed, Felister Njau, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Stella Siyao, Salome Makamba, Anatropia Theonest na Conchesta Lwamlaza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

error: Content is protected !!