Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mdee ‘amliza’ Lissu
Habari za SiasaTangulizi

Mdee ‘amliza’ Lissu

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti Chadema
Spread the love

TUNDU Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadeama), ameeleza kuumizwa na uamuzi wa Halima Mdee, aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la chama hicho (Bawacha) ‘kuasi’ chama hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

“Halima Mdee ni miongoni mwa watu ambao naye alishawahi kuteuliwa na chama kuwa mbunge wa viti maalum na utaratibu wote anaufahamu.”

“…lakini cha kushangaza ni kitu gani kimemkumba wakati huu na kwenda kinyume na utaratibu wa chama,…” alihoji Lissu wakati akifanyiwa mahojiano na televisheni moja ya mtandano.

Tayari Mdee na wenzake 18 wamefutiwa uanachama wa chama hicho kutokana na kukiuka taratibu za chama baada ya kwenda kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalumu kupitia Chadema.

Halima Mdee, Mbunge wa Chadema Viti Maalim

Kwenye mahojiano hayo, Lissu amesema, Mdee ni msomi na anafahamu vizuri taratibu zote za namna ya kupata wabunge wa viti maalumu na kwamba haelewi imekuwaje.

“Walichokifanya hawa 19 waliokwenda kuapa wamekula njama ya kukisaliti chama,” amesema Lissu ambaye aliwahi kuwa Rais wa Chama cha Mawakili Tanzania (TLS).

Lissu ambaye aligombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020 na kushika nafasi ya pili amesema, utaratibu wa kupata wabunge wa viti maalumu ndani ya chama hicho haujabadilika.

Na kwamba, utaratibu huo unaanzia Bawacha katika ngazi ya majimboni, baada ya mchakato wa huko, majina hupelekwa kwenye Kamati Kuu ambayo huteua majina matatu kutoka kila mkoa bila kujali nani alikuwa wa kwanza na nani alikuwa wa mwisho.

“Kitu cha kushangaza katika hawa wanachama 19 waliokwenda kuapa Dodoma, wengi wao wakiwa viongozi wa juu wa Bawacha ikiwa ni pamoja na Halima Mdee (mwenyekiti), Hawa Mwaifunga (makamu wake), Grace Tendega (Katibu Mkuu), nani aliyesimamia?” Amehoji Lissu.

Lissu amesema, si Chadema pekee bali vyama vyote vya siasa nchini kwa sasa, uamuzi wa majina ya viti maalumu hufanywa na viongozi wa chama husika.

“Huwezi kuwa mbunge kama hujapendekezwa na chama cha siasa,” amesema Lissu na kuongeza “namna pekee ya kiongozi wa kuchaguliwa ni kuwa mwanachama wa chama cha siasa aliyependekezwa na chama cha siasa.”

Mbali na Mdee kufukuzwa, wengi ni wale waliokuwa wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Ester Bulaya na Esther Matiko. Katibu Mkuu wa Bavicha, Nusrat Hanje. Katibu Mkuu Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Grace Tendega.

Makamu Mwenyekiti Bawacha (Bara), Hawa Mwaifunga. Naibu Katibu Mkuu Bawacha, Jesca Kishoa na Katibu Mwenezi Bawacha, Agnesta Lambat.

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa Mtwara, Tunza Malapo, Ceciia Pareso, Asia Mwadin Mohamed, Felister Njau, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Stella Siyao.Salome Makamba, Anatropia Theonest na Conchesta Lwamlaza.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!