Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Klabu ya Udasa yafungwa
ElimuHabari Mchanganyiko

Klabu ya Udasa yafungwa

Mwenyekiti wa Udasa, Dk. George Kahangwa
Spread the love

JUKWAA la wakufunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udasa) nchini Tanzania, limekana madai kuwa limefunga shughuli zake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na MwanaHALISI Online, leo Jumatano, mwenyekiti wa Udasa, Dk. George Kahangwa amesema, jumuiya hiyo haijafutwa na inaendelea na majukumu yake kama kawaida.

Amesema, “hakuna chochote kilichotokea kwa Udasa kufutwa. Udasa ni jumuiya ya wanataalamu wanaotambuliwa na Chuo Kikuu, si chombo kinachoweza kufutwa kiholela holela.”

Ameongeza, “kitu ambacho watu wanakizungumzia vibaya ni kwamba, Udasa ina Klabu na hiyo Klabu tumeisimamisha kwa muda kwa ajili ya kufanya matengenezo ambayo hayajapita hata wiki na itarejea hivi karibuni.”

Mhadhiri huyo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) amesema, “kwa hiyo, watu waje waendelee kupata huduma ya kablu hiyo itakaporejea baada ya kumalizika kwa matengenezo.”

Jumuiko la Udasa, liliundwa kwa ajili ya kusimamia haki za wakufunzi, kuratibu mambo mbalimbali yanayohusu walimu, ikiwamo maslahi yao, pamoja na kuonyesha nafasi yao kimawazo na kitaaluma kwenye jamii.

Klabu ya Udasa ambayo Dk. Kahangwa anaizungumzia kuwa imefungwa, ndio jukwaa ambalo limekuwa likitumika na wanataalamu hao kwa ajili ya kufanya mijadala mbalimbali ikiwemo kushauri, kupendekeza na hata kuikosoa Serikali.

Moja ya matukio makubwa ambayo Udasa ilifanya na kusababisha kuwapo kwa mabadiliko makubwa nchini, ni kuongoza mgomo wa mwaka 1990, ulioshirikisha walimu na wanafunzi.

Taarifa zinasema, ni kupitia mgomo huo, uliosababisha serikali kuamuru kufungwa kwa chuo kikuu cha Dar es Salaam, hatimaye serikali ilikubali kuboresha maslahi ya walimu na wanafunzi.

Aidha, Udasa imekuwa chimbuko la mijadala ya kisomi nchini Tanzania ikiwamo uanzishwaji wa mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992 pamoja na shinikizo la kuwarejesha kazini madaktari na wauguzi waliofukuzwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kufuatia mgomo wa kudai maslahi yao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!