Saturday , 25 March 2023
Home Kitengo Michezo Kigogo Yanga asimamishwa kazi
Michezo

Kigogo Yanga asimamishwa kazi

Wakili Simon Patrick
Spread the love

KAMATI ya Utendaji ya klabu ya Yanga imemsimamisha kazi Kaimu Katibu Kkuu wa klabu hiyo, Wakili Simon Patrick ambaye pia alikuwa mkurugenzi wa sheria na wanachama ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili ambazo hazikuwekwa wazi. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam …  (endelea).

Maamuzi hayo yamekuja mara baada ya kamati hiyo kufanya kikao cha dharura kilichofanyika tarehe 17 novemba 2020, kwa ajili ya kujadili swala hilo.

Katika taarifa yao ambayo imesainia na Mwenyekiti wake, Dk. Mshindo Msolla imeleza kuwa uongozi wa klabu hiyo, ili kuhakikisha haki inatendeka kamati ya utendaji itateuwa kamati huru kuchunguza jambo hili na kutoa maamuzi yenye tija kwa pande zote.

Wakili Simon amekaimu nafasi hiyo ya katibu mkuu mara baada kuondolewa kwa aliyekuwa katibu mkuu wa klabu hiyo Dk. David Luhago tarehe 16 Juni, 2020.

Kwa maamuzi hayo, Wakili Simon atakuwa katibu mkuu wa pili kuhudumu katika nafasi hiyo toka Msolla alipoingia kwenye madaraka ndani ya klabu hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Yanga: Fedha za Rais Samia zinaleta ari kubwa

Spread the loveUONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema fedha zinazotolewa na Rais...

Michezo

Simba Sc. yamvulia kofia Rais Samia, yamuahidi makubwa dhidi ya Horoya

Spread the loveWAKATI timu ya Simba ikiibuka na ushindi wa bao 3-0...

Michezo

Taasisi ya TKO na TFF yawapiga msasa makocha wa kike 54

Spread the love WAKATI Soka la wasichana likichipua kwa kasi Taasisi ya...

Michezo

Kimwanga CUP yazidi kutimua vumbi

Spread the loveMASHINDANO ya mpira wa miguu ya Kimwanga CUP ya kuwania...

error: Content is protected !!