Thursday , 9 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Mwinyi aanza kuunda serikali. ateua AG
Habari za Siasa

Rais Mwinyi aanza kuunda serikali. ateua AG

Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi
Spread the love

RAIS wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameanza kuisuka Serikali anayoiongoza kwa kumteua Dk. Mwinyi Twalib Haji kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG). Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Dk. Mwinyi amefanya uteuzi huo jana Jumanne tarehe 3 Novemba 2020 ikiwa ni siku moja imepita tangu alipoapishwa kuwa Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar.

Huu ni uteuzi wa kwanza kuufanya mara baada ya kuingia Ikulu ya Zanzibar.

Kabla ya uteuzi huo, Dk. Haji alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Dk. Mwinyi aliapishwa juzi Jumatatu tarehe 2 Novemba 2020 na Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othuman Makungu akichukua nafasi ya Dk. Ali Mohamed Shein ambaye amemaliza muda wake wa uongozi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Kuanzia Agosti marufuku kutumia mkaa, kuni

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mwendokasi Kigogo – Segerea kujengwa awamu ya 5

Spread the loveNaibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Festo Dugange...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

error: Content is protected !!