Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Magufuli kuapishwa kesho, mataifa 17 kuhudhulia
Habari za Siasa

Dk. Magufuli kuapishwa kesho, mataifa 17 kuhudhulia

Rais John Magufuli
Spread the love

SERIKALI ya Tanzania imesema, viongozi wa ngazi za juu na wawakilishi wa nchi zaidi ya 17 wamethibitisha kuhudhulia sherehe ya kumwapisha Dk. John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kesho Alhamisi tarehe 5 Novemba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Dk. Magufuli ataapishwa katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma ili kuhitimisha muhula wa pili na wa mwisho wa miaka mitano kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania inayoeleza Rais atakaa madarakani kwa miaka kumi.

Rais huyo mteule kupitia Chama tawala-CCM, alitangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC) kuwa mshindi kwa kupata kura milioni 12 sawa na asilimia 84 ya kura zilizopigwa milioni 15 huku mshindani wake, Tundu Lissu wa Chadema akipata kura milioni 1.9 sawa na asilimia 13 ya kura zote.

Leo Jumatano tarehe 4 Novemba 2020, Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Dk. Hassan Abbas akizungumza akiwa Uwanja wa Jamhuri Dodoma kunakofanyika maandalizi ya mwisho ya sherehe hizo, amesema wageni mbalimbali wamethibitisha kuhudhulia.

Dk. Abbas amesema, ni kwa mara ya kwanza sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Tanzania zinafanyikia Dodoma makao makuu ya nchi jambo ambalo ni historia inayoendana na kumuenzi Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Amesema, viongozi wa juu na wawakilishi kutoka zaidi ya mataifa 17 wamethibitisha kuhudhulia sherehe hizo zitakazoanza asubuhi.

Amewataja baadhi ya viongozi hao ni marais, Yoweri Mseveni (Uganda), Emmerson Mnangagwa (Zimbabwe), Azali Assoumani (Comoro) na Rais mstaafu wa Nageria, Olusegun Obasanjo.

Dk. Abbas ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema, Mhubiri mashuhuri raia wa Nigeria, TB Joshua naye atakuwepo, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Mabalozi,

Msemaji huyo wa Serikali amesema, kutokana na ushindi alioupata Dk. Magufuli, salamu kutoka mataifa zadi ya 32 zimetolewa na zinaendelea kutolewa.

1 Comment

  • Congratulations to you Hon. J P.Magufuli. We hope you will be more generous n responsible enough to fulfill all what you have promised during your campaigns.
    God bless you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko aipongeza GGML kudhibiti vifo, majeruhi mahali pa kazi

Spread the loveNAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za Siasa

Askofu Shoo awataka ACT kupigania maslahi ya Taifa, wasikubali kuhongwa

Spread the loveALIYEKUWA Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Askofu...

Habari za Siasa

Biteko aagiza waajiri kudhibiti vifo mahali pa kazi

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

error: Content is protected !!