Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe, Zitto, Lema waachiwa 
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe, Zitto, Lema waachiwa 

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe na wenzao wameachiwa kwa dhamana na Jeshi la Polisi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea)

Mbowe na wenzake, wameachiwa leo Jumanne tarehe 3 Novemba 2020 baada ya kushikiliwa tangu juzi usiku Jumapili katika Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Viongozi hao walikamatwa jijini Dar es Salaam kwa nyakati tofauti, wakituhumiwa.

         Soma zaidi:-

kuratibu, kuhamasisha na kuwezesha maandamano ya amani yasiyokuwa na kikomo waliyoyatangaza kuanza jana Jumatatu tarehe 2 Novemba 2020, kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba mwaka huu.

Mbali na viongozi hao, wengine ni, Godbless Lema, mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini na aliyekuwa meya wa manispaa ya ubungo, Dar es Salaam, Boniface Jacob.

Katika ukurasa wa Twitter wa Chadema umeandika “Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wajumbe wa kamati kuu, Lema na Jacob wameachiwa na Jeshi la Polisi Tanzania kwa dhamana.”

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!