Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Matokeo ya ubunge yamshtua Padri Kitima
Habari za Siasa

Matokeo ya ubunge yamshtua Padri Kitima

Padri Charles Kitima
Spread the love

MHADHIRI mstaafu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), Padri Charles Kitima amesema, Taifa la Tanzania litarudi nyuma kimaendeleo kwa sababu ya kuwa na wabunge wengi wa chama kimoja. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Padri Kitima ametoa kauli hiyo leo Ijumaa tarehe 30 Oktoba 2020 alipokuwa akizungumza na MwanaHALISI Online kuhusu matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Jumatano ya 28 Oktoba 2020 yanayoendelea kutangazwa.

Kwa mujibu wa matokeo ya ubunge yanayoendelea kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yanayoensha hadi kufikia saa 10 jioni, CCM imejikusanyia majimbo 227 kati ya 264.

Upinzani imepata viti viwili kwa maana ya Chadema kimoja na CUF kimoja.

“Dunia imezoea Tanzania ya vyama vingi na tulipokuwa na chama kimoja uchumi haukukuwa, tulipoingia vyama vingi tulipata maendeleo,” amesema Padri Kitima.

Padri Kitima amesema, kitendo cha Bunge kuwa na idadi kubwa ya wabunge wa chama kimoja, hakutakuwa na kupingana kwa hoja, bali maamuzi yatakayofanyika yatakuwa na mlengo wa chama kimoja.

Joseph Haule

“Tunashikiniza watu kuachana na vyama vingi kiasi fulani, kwa Bunge chama kikiwa kimoja hakuna kupingana, kwa dunia ya sasa si vizuri. Tunakuwa na Bunge lenye watu wanaofikiri kwa mtazamano mmoja,” amesema Padri Kitima.

“Katika uchaguzi wa kwetu, nia za watu hazijaheshimiwa, si vizuri kwani tutakuwa na bunge ambalo haingalii dunia inataka nini mfano China ina chama kimoja lakini nia za watu huheshemiwa, katika uchaguzi wa kwetu nia za watu hazijaheshimiwa, si vizuri tutakuwa na bunge ambalo haiangalii dunia inataka nini,” amesema Padri Kitima.

Padri Kitima ambaye ni Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) amesema, matokeo ya uchaguzi wa wabunge na madiwani yatasababisha baadhi ya wananchi kukosa wawakilishi wanaowataka.

“Hasara ya kukosa  wabunge aina fulani waliokuwa na matarajio nao,  sababu sio lazima wote wanaopiga kura wanategemea watu wao wapite bali wanategemea mtu fulani akiwepo bungeni atawawakilisha,” amesema Padri Kitima.

Aidha, Padri Kitima amesema bunge lijalo litakosa mawazo mbadala kutoka vyama vingine.

“Tunakoelekea tuna bunge la chama kimoja na tulishazoea kwa miaka 25 kuwa na mawazo mbadala kutoka vyama vingine, lakini sasa katika Bunge lijalo hatutakuwa nayo,” amesema  Padri Kitima.

Kwa matokeo yaliyokwisha kutangazwa, vigogo wa upinzani wakiongozwa na aliyekuwa kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, Freeman Mbowe ameshindwa ubunge Hai Mkoa wa Kilimanjaro kupitia Chadema.

Zitto Kabwe

Wabunge wengine ambao wameshindwa na kuzua mijadala sehemu mbalimbali ni; Zitto Kabwe (Kigoma Mjini-ACT-Wazalendo), Godbless Lema (Arusha Mjini), Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini) na Joseph Mbilinyi maarufu Sugu (Mbeya Mjini).

Wengine ni; Halima Mdee (Kawe), Esther Matiko (Tarime Mjini), John Heche (Tarime Vijijini) na Saed Kubenea wa Kinondoni kupitia ACT-Wazalendo.

Pia kuna, James Mbatia (Vunjo), Joseph Selasini (Rombo) na Anthony Komu (Moshi Vijijini) wote kutoka NCCR-Mageuzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

error: Content is protected !!