Sunday , 2 April 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Singida hawategemei alizeti pekee
Habari Mchanganyiko

Singida hawategemei alizeti pekee

mazao la Alizeti
Spread the love

IMEELEZWA kuwa mabadiliko ya kimaisha na kiuchumi ya wakazi na mkoa wa Singida hayatokani na kilimo cha zao la alizeti pekee bali yapo mazao mengine wanayolima sambamba na shughuli za kiuchumi. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Mtafiti wa masuala ya Kilimo kutoka chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kupitia mradi wa utafiti wa Sera za Kilimo barani Afrika (APRA) Dk. Christopher Magomba alisema Kilimo cha mazao mengine na shughuli nyingine za kiuchumi ikiwemo miradi midogomidogo imekuwa chanzo mbadala cha uchumi.

Alisema wakazi wa mkoa huo wamekuwa wakijishughulisha na kilimo cha mazao mengine zaidi ya alizeti ikiwemo mahindi, vitunguu, nyanya, mtama na pamba.

“Mfano mzuri ni kilimo cha mahindi ambacho kinazalishwa kwa asilimia 83.86 na kuwa ni moja ya zao linaloonesha kuchangia maendeleo ya Singida ambayo hailingani na alizeti ambayo kiutafiti imeonesha kuwa na asilimia 71 tu,” alisema.

Naye mkuu wa miradi huo wa APRA, Profesa Aida Isinika, alisema suala la maendeleo mkoani Singida ikiwemo ujenzi wa nyumba nzuri na za kisasa linatokana na kutanuka kwa suala zima la kilimo kutokana na wakazi hao kuongeza kulima mazao mengine ya kilimo na biashara na kupilunguza kulima zao moja la alizeti pekee kama ilivyokuwa miaka ya 1970.

Pia Prof. Isinika alisema vijana wengi katika miaka ya sasa wamekuwa wakipenda kulima kilimo chenye tija na soko kama vile mpunga, vitungii, nyanya na mazao mengine.

Alisema suala la utoaji wa ajira katika mashamba hayo linafanywa na wakulima wa kati kwa kuwapa vibarua vijana wenzao ukilinganisha na wawekezaji wakubwa waliopo kwenye mashamba mbalimbali.

Akiwasilisha mada kuhusu matokeo ya utafiti uliohusu ushiriki wa vijana kwenye kilimo biashara kwenye bonde la kilombero, Profesa Ntengua Mdoe alisema vijana wa umri wa kati ya miaka 15-35 ambao ni sawa na asilimia 35.5 ndiyo wenye kunufaika zaidi katika bonde hilo ukilinganisha na makundi mengine.

Hivyo alisema kipato wanachopata vijana hao wanaoshughulika na kilimo ni kikubwa kuliko nguvu inayowekezwa na vijana wanaofanya kazi zingine nchini.

Profesa Mdoe alizishauri halmashauri xa wilaya na serikali za mitaa kitenga ardhi ya kilimo kwa ajili ya vijana kama ilivyoelekezwa kwenye sheria ya ardhi ya mwaka 1999 sambamba na kuwasaidia mikopo kupitia mfuko wa maendeleo ya vijana wa asilimia 4 unaotoka kwenye mapato ya Halmashauri.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Ditopile aungana na Wana-Kongwa kwa Iftar, wamuombea dua Rais Samia

Spread the loveKATIKA muendelezo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Mbunge wa Viti...

Habari Mchanganyiko

PSSSF yawekeza kwenye viwanda 4, kuzalisha ajira 3,000

Spread the loveKATIKA kuisaidia Serikali kupunguza tatizo la uhaba wa ajira nchini,...

Habari Mchanganyiko

Luhemeja ahimiza utunzaji rasilimali maji kwa faida ya vizazi vijavyo

Spread the love  NAIBU Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja...

Habari Mchanganyiko

NSSF yawapa darasa wahariri uwekezaji wa nyumba, yapewa cheti

Spread the loveMFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umetoa wito...

error: Content is protected !!