Wednesday , 8 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto: Tumedhibiti kura feki, mapambano bado
Habari za Siasa

Zitto: Tumedhibiti kura feki, mapambano bado

Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo
Spread the love

ZITTO Kabwe, mgombea ubunge Kigoma Mjini kupitia ACT-Wazalendo amesema ‘tumedhibiti wizi.’ Anaripoti Yusuph Katimba, Kigoma … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari Jumatano leo tarehe 28 Oktoba 2020 katika kituocha kupigia kura Cha Shule ya Msingi Mnarani, Kigoma Ujiji amesema, amekamata kura nyingi kwenye vituo mbalimbali jimboni humo.

Na kwamba, kuanzia asubuhi amekuwa akitembelea vituo mbalimbali kujua hali halisi.

“Kata ya Katubuka tumekamata kura nyingi, tumekamata kura 3,000 ambazo tayari zimepigwa, hiyo ni kata moja.”

“Ushahuda wa kura katika kata zingine tunao, mfano kura hizi hapa (anazionesha msaidizi wake), tumeishatoa taarifa katika mamlaka husika,” amesema.

Amesema, tayari wamedhudhibiti kura nyingi ambazo zilikuwa kwenye mpango wakuingizwa kwenye vituo vya kura.

“Tumedhibiti kura zaidi ya 12,000, tunaendelea kutembelea vituo vingine. Hili tunalisema kama ushahudi, wajue hivyo,” amesema Zitto huku akisisitiza wanaendeleza mapambano ya kuzuia kura hizo feki

Issa Bukuku Ofisa Uchaguzi Jimbo la Kigoma Mjini amesema taarifa za kupenyeza kura amezipata.

Amesema, moja ya kata iliyolalamikiwa na Zitto, Kata ya Kasingirima ni kwamba vurugu hizo zilikuwepo.

“Kwenye kata hiyo ni kweli nimekuta vurugu, huyo anayedaiwa kuwa na kura nimeiona na huo mkoba,” amesema Bukuku.

Amesema, licha ya kumuona lakini hakwenda kuukagua huo mkoba ili kuthibitisha madai ya Zitto.

Alisema, hakufanya hivyo kwa kuwa mtu huyo alikuwa mikononi mwa polisi.

Akiulizwa kuhusu tukio hilo, Mkuu wa Polisi Kigoma, RPC James Manyama amesema, hayupo mjini.

“Sina taarifa hizo,maana sipo Mjini. Nipo Kasulu, nitafuatilia kujua ukweli wake,” amesema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Kuanzia Agosti marufuku kutumia mkaa, kuni

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mwendokasi Kigogo – Segerea kujengwa awamu ya 5

Spread the loveNaibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Festo Dugange...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

error: Content is protected !!