Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Polisi yazungumzia waliobeba vibegi vituoni
Habari za Siasa

Polisi yazungumzia waliobeba vibegi vituoni

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa
Spread the love

KAMANDA wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amezungumzia baadhi ya watu kuonekana wakiwa na mabegi mgongoni katika maeneo ya vituo vya kupigia kura. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Mambosasa amesema hayo leo Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020 wakati akizungumzia hali ya usalama katika jiji hilo.

Amesema sio kosa kwa mwananchi kubeba begi, kwa kuwa baadhi ya watu wanalazimika kubeba mabegi kwani wanatokea mikoa mingine kuja kupiga kura Dar es Salaam ambako wamejiandikisha kupiga kura.

Kamanda Mambosasa ametoa ufafanuzi huo baada ya Mgombea  Ubunge wa Kawe kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Halima Mdee kuzua sintofahamu katika Kituo cha Kawe akidai kuna watu wamebeba mabegi yenye kura za kughushi.

Kamanda Mambosasa amesema, tukio hilo ni la kihuni kwa kuwa Mdee hakuwa na mamlaka ya kuzuia watu wasipige kura.

“Wako watu wamesafiri kutoka mikoani kuja kupiga kura sababu alijiandikishia Dar es Salaam, akitoka kumaliza kura anarudi alikotokea,” amesema Mambosasa

Amesema, “kupiga marufuku mtu asiende na begi ni cha kihuni lakini mbaya zaidi alikwenda mbali yeye sio tume akazuia watu wasipige kura. Tulimuonya hayo aliyoyafanya hayamletei heshima.”

Hata hivyo, Kamanda Mambosasa amesema kama Jeshi la Polisi litapokea malalamiko hayo litafungua jalada la upelelezi na kama ikithibitika kuna jinai tukio la kisheria litachukuliwa.

“Madai hayajaletwa kwangu viongozi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wanasema ni maneno ya mtaani, ikithibitika tutafungua jalada, tutapeleleza na kuangalia kama kuna jinai, ikithibitika hatua za kisheria zitachukuliwa,” amesema Kamanda Mambosasa.

Katika moja ya kituo cha kupigia kura cha Jimbo la Kawe, Mdee alidai kuna kura feki zimepigwa hivyo kutaka kuzitoa, hali iliyozua tafrani na polisi walimkamata kwa mahojiano kisha akaachiwa.

Aidha, Kamanda Mambosasa amesema Jeshi hilo limemkamata kijana mmoja akiwa na begi ambalo ndani yake kulikuwa na kisu na sare za mgambo.

Pia, linanshikilia kijana mmoja kwa tuhuma za kufanya vurugu kituoni.

“Kimara alikamatwa kijana  mmoja alikuwa na begi ndani kuna kisu na sare, Mbagala kuna kijana alivamia kwenye kituo akapiga picha si mwandishi alikwenda pale kutengeneza vurugu, tumemkamata kwa ajili ya kuingia kwenye kituo sababu aliyetakiwa kuingia ni wakala,” amesema Kamanda Mambosasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!