Thursday , 9 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mvua Dar: Tahadhari yatolewa
Habari Mchanganyiko

Mvua Dar: Tahadhari yatolewa

Spread the love

WAKAZI wa Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani, wametakiwa kuchukua tahadhari ya magonjwa ya mlipuko kutokana na mvua  zinazoendelea kunyesha. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam…(endelea).

Tahadhari hiyo imetolewa na Prof. Abel Makubi, Mganga Mkuu wa Serikali leo tarehe 15 Oktoba 2020 na kwamba, kuwa uwezekano wa mvua hizo kuibua magonjwa ya Kipindupindu, Kuhara damu pamoja na yale yanayoambikizwa na Mbu ikiwemo Maralia na Dengue.

Prof. Makubi amesema, ugonjwa wa kipindupindu ulikoma Julai   2019 kutokana na jitihada  na maboresho ya miundombinu sambamba na kuongezeka kiwango cha upatikanaji wa maji safi na salama.

“Tuzingatie kuchemsha maji ya kunywa au kutibu kwa dawa maalum kama Waterguard na nyingine kabla ya kuyatumia, pia kuhakikisha yanahifadhiwa katika vyombo safi.

“Tuepuke kula chakula kikichopoa au kuandaliwa katika mazingira yasiyo salama, tunawe mikono kwa maji tiririka na sabuni mara kwa mara, kabla ya kula na baada ya kutoka chooni ama baada ya kumnawisha mtoto aliyejisaidia,” ameeleza kwenye taarifa yake.

Prof. Makubi amewataka watu kuongeza usimamizi wa usafi wa jumla na mikono katika mikusanyiko ikiwemo shuleni na masokoni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

Kengold wakabidhiwa kombe NBC Championship

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) Benki...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

error: Content is protected !!