WAKAZI wa Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani, wametakiwa kuchukua tahadhari ya magonjwa ya mlipuko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam…(endelea).
Tahadhari hiyo imetolewa na Prof. Abel Makubi, Mganga Mkuu wa Serikali leo tarehe 15 Oktoba 2020 na kwamba, kuwa uwezekano wa mvua hizo kuibua magonjwa ya Kipindupindu, Kuhara damu pamoja na yale yanayoambikizwa na Mbu ikiwemo Maralia na Dengue.
Prof. Makubi amesema, ugonjwa wa kipindupindu ulikoma Julai 2019 kutokana na jitihada na maboresho ya miundombinu sambamba na kuongezeka kiwango cha upatikanaji wa maji safi na salama.
“Tuzingatie kuchemsha maji ya kunywa au kutibu kwa dawa maalum kama Waterguard na nyingine kabla ya kuyatumia, pia kuhakikisha yanahifadhiwa katika vyombo safi.
“Tuepuke kula chakula kikichopoa au kuandaliwa katika mazingira yasiyo salama, tunawe mikono kwa maji tiririka na sabuni mara kwa mara, kabla ya kula na baada ya kutoka chooni ama baada ya kumnawisha mtoto aliyejisaidia,” ameeleza kwenye taarifa yake.
Prof. Makubi amewataka watu kuongeza usimamizi wa usafi wa jumla na mikono katika mikusanyiko ikiwemo shuleni na masokoni.
Leave a comment