Friday , 9 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif: Vijana wapo tayari
Habari za SiasaTangulizi

Maalim Seif: Vijana wapo tayari

Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo
Spread the love

MAALIM Seif Shariff Hamad, mgombea urais visiwani Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, amesema safari hii vijana wapo tayari. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).

“Tunapambana na CCM (Chama Cha Mapinduzi) na nafikiri vijana wengi safari hii wamejipanga na kujiandaa, likitokea lolote wapo tayari,” amesema Maalim Seif wakati akizungumza na gazeti moja la kila wiki, mapema wiki hii.

Akizungumzia ushindani uliopo kati yake na CCM, amesema ndani ya chama hicho, wapo wanaomuunga mkono kutokana na kutoridhishwa na mgombea aliyeteuliwa na chama hicho.

Mgombea aliyeteuliwa na CCM kugombea urais Zanzibar NI Dk. Hussein Ali Mwinyi na kwamba, anajua hapambani na Dk. Mwinyi pekee bali CCM wote.

“Tofauti iliyopo baina ya chaguzi zote hizo ni ndogo sana, kwa sababu chaguzi zote hizi tunashindana na wagombea wa CCM. na CCM ni ile ile na kwa kweli unaposhindana na CCM hushindani na mgombea, unashindana na CCM wote.

“…tofauti iliyopo  kubwa hivi sasa ndani ya CCM , hakuna ule umoja ambao walikuwa nao zamani. Watu wengi sasa hivi hawaridhishi na mgombea aliyeletwa na chama chao kuwania nafasi hiyo,” amesema Maalim Seif.

kwa hiyo, kidogo inatufanya tuamini kwamba kuna watu wengi wanaotuunga mkono ndani ya CCM.

Akizungumzia kauli ya kwamba yeye ni ‘mgombea mzoefu wa kushindwa’ amesema yeye si mzoefu wa kushindwa bali mzoefu wa kudanganywa.

“…sidhani kama mimi ni mzoefu wa kushindwa, lakini mimi ni mzoefu wa kudanganywa, kuanzia mwaka 1995, 2000, 2005, 2010 na hata 2015 nimekuwa nikishinda na ushahidi kamili ulipatikana mwaka 2015.

“Na hii kila mmoja alijua kama tumeshinda tena kwa kura nyingi sana, lakini mwenyekiti wa tume akapata maagizo ya kuwa afute uchaguzi kinyume cha Katiba na sheria, kwa hiyo kwamba nashindwa aaaah! nanyang’anywa,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaTangulizi

Ngoma bado mbichi mkataba wa Bandari

Spread the love  SAKATA la mkataba wa uendeshaji, uendelezaji na uboreshaji wa...

BiasharaTangulizi

Mkurugenzi TPA: Mkataba unaweza kuvunjwa

Spread the loveMKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA),...

BiasharaTangulizi

Mkurugenzi TPA: Mikataba ya utekelezaji bado haijasainiwa

Spread the loveMKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA),...

Habari za Siasa

Lussu: Mkataba wa DP bandarini si wa miaka 100

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesema hakuna ukweli wowote...

error: Content is protected !!