MAALIM Seif Sharif Hamadi, mgombea urais visiwani Zanzibar amesema, Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) inataka kumfungia kama Tundu Lissu, mgombea urais Tanzania kupitia Chadema alivyofungiwa kufanya kampeni kwa siku saba. Anaandika Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).
Ni baada ya Kamati ya Maadili ya ZEC kumtaka kufika mbele yake leo tarehe 15 Oktoba 2020 kujibu tuhuma zilizowasilishwa na Chama cha Demokrasia Makini kwamba, anashawishi wafuasi wake kupiga kura tarehe 27 Oktoba 2020 badala ya tarehe 28 Oktoba 2020.
“…nimetakiwa nifike Kamati ya Maadili ya ZEC. Eti nimelalamikiwa na Chama cha Demokrasia Makini kwa kuwaambia watu wakapige kura Oktoba 27.

‘Wanataka kuni-Lissu. Hawa wanatumika na CCM. Kama Mwinyi (Dk. Hussein Mwinyi, mgombea urais Zanzibar kupitia CCM) ana hoja akajibu jukwaani. Narudia sote tukapige kura Oktoba 27,” ameandika Maalim Seif.
Sheria ya Uchaguzi Zanzibar imeweka utaratibu kwa baadhi ya watumishi wa umma hasa wanaosimamia siku ya uchaguzi, kupiga kura siku moja kabla ya siku ya uchaguzi husika.
Hivi vyama uhange vya upinzani vimetoka wapi? Nani amevitengeneza?
Axnteni kwa taarifa muhimu kama hizi,