Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wazee waja juu, wamkingia kifua Lissu
Habari za Siasa

Wazee waja juu, wamkingia kifua Lissu

Spread the love

HATUA ya Jeshi la Polisi nchini Tanzania kumzuia Tundu Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuzungumza na wananchi akiwa njiani, imepingwa na Baraza la Wazee wa chama hicho (BAZECHA). Anaripoti Hamisi Mguta, Dar es Salaam…(endelea).

Wamesema, kinachofanyika sasa kwa wagombea wa chama hicho kuanzia ngazi ya urais, ubunge na udiwani kinakwenda kinyume na ahadi ya Rais John Magufuli kwamba, uchaguzi mkuu utakuwa huru na haki.

Hashim Issa, mwenyekiti wa baraza hilo akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi tarehe 1 Oktoba 2020, makao makuu ya chama hicho Kinondoni, jijini Dar es Salaam, amehojia msingi wa kauli ya Rais Magufuli ya ‘uchaguzi huru na haki’ na kile kinachoendelea nchini.

“Wazee wa Chadema tunasikitika, rais alisema uchaguzi utakuwa wa huru na haki, lakini tumeona figisu wanazofanyiwa wagombea wetu katika kampeni,” amesema mwenyekiti huyo.

Ameeleza kulalamikia hatua iliyochukuliwa na Jeshi la Polisi kumzuia Lissu na mgombea mwenza Salum Mwalimu kuzungumza na wananchi kama ilivyo kwa mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli.

Tarehe 28 Septemba 2020, msafara wa Lissu ulikumbana na hekaheka za mabomu ya machozi pale alipotaka kusalimia wananchi waliokusanyika barabarani eneo la Nyamongo, Tarime vijijini mkoani Mara wakimsubiri awasalimie.

Pia, Polisi Ifakara mkoani Morogoro, walivamia msafara wa Mwalim na kupiga mabomu ya machozi wakati alipotaka kusalimia wananchi aliowakuta barabarani.

Polisi walimlazimisha Mwalimu kuendelea na safari bila kusalimia wananchi hao.

Katika hatua nyingine, BAZECHA wameilalamikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kwamba imeengua wagomea wake bila sababu za msingi.

Wameeleza kuitaka NEC kurejesha wagombea wake ili kutengeneza uwanda sawa wa mapambano ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

“Tunaitaka Tume ya Uchaguzi iwarudishe mara moja wagombea wetu wa ubunge na udiwani walioenguliwa bila sababu za msingi,” amesema Hashim.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mpina mwiba CCM, ahofia kuzibwa mdomo

Spread the loveWAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM), kikijinasibu kuwa kinara wa demokrasia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mabeyo ametuepusha

Spread the loveNIMEGUSWA na uadilifu, utiifu na uaminifu wa Mkuu mstaafu wa...

Habari za SiasaTangulizi

CCM yaitaka TAKUKURU kuichunguza Chadema tuhuma alizoibua Lissu

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana...

error: Content is protected !!