May 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Papa Francis ‘amtimua’ Pompeo

Spread the love

MIKE Pompeo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amegomewa kukutana na Papa Francis, Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Dunani. Inaripoti Shirika la Habari la Uingereza (BBC)…endelea.

Hatua hiyo inatokana na msimamo wa Papa Francis kueleza kwamba, katika kipindi hiki cha kampeni za Marekani, kiongozi huyo hatokutana na mwanasiasa yeyote.

Waziri huyo inaelezwa, alitaka kwenda kuonana na Papa Francis ‘kuweka sawa mambo’ baada ya kutoa kauli iliyokasirisha Vatcan kwamba, kanisa hilo linapoteza mamlaka yake ya kinidhamu kwa kufanya makubaliano mapya na China kuhusu uteuzi wa maaskofu.

Na kwamba, mgogoro wa kidiplomasia kati ya China na Marekani ndio uliomsukuma Pompeo kutaka kuitumbukiza Vatcan na kulichafua kanisa hilo mbele ya uso wa dunia.

Vatican imemkatalia waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Mike Pompeo kuonana na Papa Francis.

Kiongozi huyo wa juu wa Kanisa Katoliki ameelezwa hawapokei wanasiasa wakati wa kipindi cha uchaguzi.

Hatua hiyo inaongeza hali ya mzozo wa kidiplomasia baada ya kauli ya Pompeo kuhusu China na Kanisa Katoliki.

Mwaka 2018 Vatican ilifanya makubaliano na China kuwa na maoni juu ya uteuzi wa maaskofu wa China.

Wakati huo huo, Papa Francis alisema, mpango huo utaponya vidonda vya zamani na kuleta umoja kamili wa Kikatoliki nchini China.

Makundi ya haki za binadamu yamekuwa yakieleza kwamba, Wakatoliki wengi nchini China, wanateswa kwa kuahidi utii kwa Papa badala ya chama rasmi cha Wakatoliki nchini China.

error: Content is protected !!