Tuesday , 21 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Tamwa yazindua ‘wanawake wanaweza’
Habari Mchanganyiko

Tamwa yazindua ‘wanawake wanaweza’

Spread the love

CHAMA cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa) kimeanza utekelezaji wa mradi wa ‘Wanawake Wanaweza’ uliofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wanawake (UN-Women). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea)

Lengo wa mradi huo ni utetezi wa haki za wanawake na watoto, kuongeza ushiriki wa wanawake katika uongozi, kuondoa mifumo kandamizi inayochochea ukatili kwa makundi maalum kwa kutumia vyombo vya habari.

Mradi huo wa mwaka mmoja ulioanza Agosti 2020, umezinduliwa rasmi leo Alhamisi tarehe 1 Oktoba 2020 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa, Rose Reuben.

Rose amesema, mradi huo, utaongeza uelewa kwa umma kuhusu umuhimu kuhusu ushiriki wa wanawake kwenye siasa, uongozi na madhara ya magonjwa ya mlipuko kama COVID-19 kwa wanawake na wasichana.

Amesema, ili kufanikisha lengo kuu la mradi huo, Tamwa itawajengea uwezo wanahabari katika kuripoti habari za jinsia na ufuatiliaji wa ushiriki wa wanawake kwenye uongozi na siasa.

Pia, midahalo ya kihabari kwa ajili ya kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu umuhimu wa ushiriki wa wanawake katika siasa na uongozi itafanyika.

Rose amesema, mikoa 16 itahusika kwenye mradi ambayo ni; Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Mara, Mbeya, Ruvuma, Lindi na Mwara.

Amesema, wilaya 112 za mikoa hiyo na kata 458 ndiyo maeneo yatakayotumika kama sampuli ya utekelezaji wa malengo ya mradi huo.

Mkurugenzi huyo amesema, Tamwa inatambua ushiriki wa wanawake katika nafasi za maamuzi hasa za kisiasa bado ni mdogo, hali ambayo inakinzana na azma ya kujenga jamii isiyokuwa na ubaguzi kama ilivyobainishwa kwenye dira ya Taifa 2025, Katiba ya Tanzania ya mwaka 1997 pamoja na sharia mbalimbali za nchi.

“Kwa mfano, ripoti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC:2016) inaonyesha asilimia 17 ya mawaziri ni wanawake, makatibu wakuu wanawake ni asilimia 11, wakuu wa mikoa ni asilimia 23, wakuu wa wilaya ni asilimia 28 na hii inaonyesha bado nafasi ya mwanamke katika ngazi za uongozi ni mdogo.”

“Hata hivyo, bado tunaupongeza uongozi wa awamu ya tano, kwa mara ya kwanza alichaguliwa Makamu wa Rais mwanamke, Samia Suluhu Hassan,” amesema Rose

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tanzania yakabidhi rasmi msaada nchini Malawi

Spread the loveWAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,...

Habari Mchanganyiko

Bashe: Tumeshagawa pikipiki 5,500 kati ya 7,000 kwa maafisa ugani

Spread the love  WAZIRI wa Kilimo, Hussen Bashe, amesema wizara hiyo tayari...

Habari Mchanganyiko

Spika Tulia awapa neno mawaziri utekelezaji mashamba ya pamoja

Spread the love  SPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, amewataka mawaziri kushirikiana...

Habari Mchanganyiko

Ukosefu wa maadili kwa wakunga, wauguzi bado changamoto

Spread the loveIMEELEZWA kuwa vitendo vya uvunjifu wa maadili kwa  wauguzi na...

error: Content is protected !!