Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Fatma Karume ang’olewa TLS, asema…
Habari za Siasa

Fatma Karume ang’olewa TLS, asema…

Fatma Karume
Spread the love

KAMATI ya Maadili ya Mawakili Tanganyika imemkuta na hatia, Fatma Karume ya kukiuka maadili ya uwakili hivyo kuamlu jina lake (namba 848) kuondolewa katika orodha ya mawakili wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatano tarehe 23 Oktoba 2020 ikiwa imepita mwaka mmoja tangu Mahakama Kuu ya Tanzania kumsimamisha uwakili ikimtuhumu kutoa matamshi yaliyolalamikiwa na Serikali.

Tarehe 20 Septemba 2019, Mahakama Kuu ya Tanzania ilitoa uamuzi huo wa kumsimamisha na kupeleka suala hilo, Kamati ya Maadili ya Mawakili Tanganyika kwa hatua zaidi.

        Soma zaidi:-

Fatma alikutwa na tuhuma hizo alipokuwa akimtetea aliyekuwa Katibu Mwenezi wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu katika kesi aliyoifungua mahakamani hapo kupinga uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Profesa Adelardus Kilangi.

Fatma, ambaye ni ni mtoto wa Rais mstaafu wa Zanzibar, Aman Abei Karume alilalamikiwa na upande wa Serikali katika kesi hiyo juu ya matamshi yake. Uamuzi huo ulitolewa na Jaji Kiongozi wa Tanzania, Dk. Eliezer Feleshi ambaye pia aliiondoa kesi hiyo.

Baada ya kutoka kwa uamuzi huo wa kumwondoa TLS, Fatma aliyepata kura Rais wa TLS kati ya mwaka 2018/19 ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba hatokataa rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Fatma Karume

MwanaHalisi Online limezungumza na Rais wa TLS, Rugemeleza Nshala kujua utekelezaji wa uamuzi huo ambapo amesema “ninazo taarifa hizo lakini bado sijapokea taarifa rasmi na mhusika anaweza kukata rufaa kama hajaridhishwa na uamuzi huo.”

Kung’olewa kwa Fatma TLS kunakuja ikiwa ni siku kadhaa zimepita  tangu Kampuni ya Uanasheria ya IMMMA aliyoshiriki kuianzisha kumfukuza kazi.

Barua ya Kampuni ya IMMMA ya tarehe 16 Septemba 2020 iliyosainiwa na Sadock Magai, Mkurugenzi Mwenza wa kampuni hiyo ilisema, Fatma ameondolewa katika sehemu ya umiliki wa kampuni baada ya mkabata wake alioingia tarehe 26 Machi 2007 kuvunjwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!