Saturday , 3 June 2023
Home Habari Mchanganyiko TASUWORI kuunganisha vijana 300
Habari Mchanganyiko

TASUWORI kuunganisha vijana 300

Spread the love

SHIRIKA la linalojishughulisha na Kulinda na Kutetea Haki za Wanawake Tanzania (TASUWORI), limeeleza kuwa tayari kuunganisha vijana 300 kutoka kwenye vikundi tisa vinavyofanya shughuli za kiuchumi wilayani Gairo, Morogoro.  Anaripoti Christina Haule, Morogoro…(endelea).

Emmanuel Mapigano, mkurugenzi wa shirika hilo ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari mbele ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Agnes Mkandya.

Amesema, vikundi sita kati ya tisa tayari vinaendesha miradi mbalimbali ya kiuchumi na vimesajiliwa na halmashauri katika kupewa mikopo mbalimbali.

Amesema, kufuatia utayari huo, shirika hilo litaendelea kutoa elimu za mbinu mbalimbali za kukua kiuchumi ikiwemo kutengeneza jam, maziwa na wine za aina mbalimbali.

Mapigano amesema, wanatarajia kuviunganisha vikundi hivyo na taasisi za kifedha ikiwemo PASS na Benki ya NMB ili waweze kupata mikopo na kufikia hatua ya kujiendesha vizuri kibiashara.

Amesema, vikundi hivyo sita vimeanzisha miradi ya ufugaji kuku, ufugaji nguruwe, kilimo cha bustani, kilimo cha mbogamboga, kilimo cha mahindi na utengenezaji wa wine.

 “Zipo taasisi nyingi zenye miradi ya mikopo kwa vijana ikiwemo mradi wa uwezeshaji kiuchumi unaofadhiliwa na SWISS Contact,” amesema na kungeza “jukumu lao vijana kujitahidi tu kuanzisha miradi inayoeleweka,” amesema Mapigano.  

Mapigano amesema, vijana hao wenye umri wa miaka 16 – 24, wameanzisha miradi hiyo wanayoiendesha wenyewe ambayo inawapa moyo wa kujidhatiti kwenye masuala ya uongozi kutokana na kusimamia wenyewe.

Mkurugenzi Mkandya amesema, halmashauri kuna mikopo ya asilimi 10 ambapo asilimia nne hutengwa kwa ajili ya vijana, asilimia nne kwa ajili ya wanawake na asilimia mbili kwa ajili ya watu wenye ulemavu.

Amesema, bado kuna changamoto kwa vijana kujitokeza kuchukua mikopo hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Magunia 731 ya bangi yakamatwa, mamia ya hekari yateketezwa Arumeru

Spread the love  MAMIA ya magunia ya madawa ya kulevya aina ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Bosi NIC apandishwa kizimbani, akabiliwa na mashitaka 365

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa...

Habari Mchanganyiko

Serikali yakabidhi eneo la mahakama ya Afrika ya haki za binadamu

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa...

Habari Mchanganyiko

Udhamini wa NMB mikutano ya ALAT wafikia 1.2 bilioni

Spread the loveBENKI ya NMB imeendelea kufanya kazi kwa karibu na Asasi...

error: Content is protected !!