Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Jaji Mkuu: Kesi za uchaguzi zisicheleweshwe
Habari za Siasa

Jaji Mkuu: Kesi za uchaguzi zisicheleweshwe

Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma
Spread the love

MAJAJI wa Mahakama ya Rufani Tanzania wametakuwa kutochelewesha kutoa uamuzi wa kesi za kisiasa pasipo na sababu za msingi kwa kuwa, huwa na mvuto kwa wananchi. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Prof. Ibrahim Hamis Juma, Jaji Mkuu wa Tanzania ametoa kauli hiyo leo Jumatano tarehe 2 Agosti 2020, mkoani Morogoro wakati akifungua Programu ya mfunzo ya namna bora ya uendeshaji wa mashauri ya uchaguzi.

Programu hiyo imelenga kuwaweka majaji katika utayari wa kupokea, kusikiliza na kukamilisha mashauri ya uchaguzi ndani ya muda mfupi ambayo ni sehemu muhimu ya kuimarisha uchaguzi ulio huru na haki.

Amesema, kazi na uamuzi wao wa kijaji uongozwe na sheria pia ustadi na si vinginevyo.

“Waheshmiwa majaji wana majukumu ya kuhamasisha kupitia waendeshaji wa mashauri, kuonesha kuwa mfano wa kusikiliza ama kutoa maamuzi katika mashauri ya uchaguzi na kutoa picha kuwa, mahakama ni sehemu huru na ya haki,” amesema.

Amesema, mashauri ya uchaguzi huwa na mvuto mkubwa kwa wananchi na kwamba, ingawa wananchi wengine huwa hawafuatilii mashauri ya kawaida ya jinai na madai, hali hubadilika wakati wa kesi za uchaguzi.

“Majaji na mahakimu wanatakiwa kutambua kuwa, mashauri ya uchaguzi ni nafasi nadra sana kwa wananchi kuwapima na kuwatathmini katika maeneo mbalimbali ya utoaji haki ikiwemo
kwa kiasi gani wapo huru, uhuru wa mahakama kwa ujumla.”

“Wananachi watafuatilia taratibu zote za kesi za uchaguzi kuanzia kusikiliza maoni na kufuatilia gharama za kesi, hata jaji au hakimu anavyoendesha mashauri mahakamani,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mpina mwiba CCM, ahofia kuzibwa mdomo

Spread the loveWAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM), kikijinasibu kuwa kinara wa demokrasia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mabeyo ametuepusha

Spread the loveNIMEGUSWA na uadilifu, utiifu na uaminifu wa Mkuu mstaafu wa...

Habari za SiasaTangulizi

CCM yaitaka TAKUKURU kuichunguza Chadema tuhuma alizoibua Lissu

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana...

error: Content is protected !!