Tuesday , 30 April 2024
Home Habari Mchanganyiko TASAF kutambua kaya maskini kielektroniki
Habari Mchanganyiko

TASAF kutambua kaya maskini kielektroniki

Mkurugenzi wa TASAF, Ladislaus Mwamanga
Spread the love

MFUKO wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) umejipanga kutumia mfumo wa kielektroniki katika kuhakiki na kuzipata kaya maskini kwenye kipindi cha pili ya mpango wa kunusuru kaya maskini wa TASAF III ili kuondokana na kuingiza wasio maskini katika mpango huo na kuwapata walengwa sahihi. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Mkurugenzi wa TASAF, Ladislaus Mwamanga alisema hayo mjini Morogoro katika kikao kazi baina  ya wahariri wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari nchini na TASAF.

Aidha alisema mfumo huo katika utawafanya kubaini watu ambao hawana sifa pamoja na wale ambao wameshafariki dunia na kuwaondoa kwenye kunufaika na mpango huo.

Mwamanga alisema TASAF  awamu ya tatu kipindi cha pili itatumia kiasi cha shilingi trilioni 2 kwa kipindi cha miaka minne ambapo itazifikia Halmashauri na wilaya 185 Tanzania Bara na Visiwani.

“Katika awamu ya tatu kipindi cha kwanza utekelezaji wake ulifanikiwa kwa asilimia 70, na zilitumika shilingi trilioni 1.7  kwa miaka saba na sasa tunaendelea kuhawilisha,” alisema.

Hata hivyo alisema zaidi ya kaya 1,320 zilijitoa zenyewe baada ya kuona zinajitosheleza kiuwezo kufuatia kupokea fedha za uhawilishaji katika kipindi cha TASAF II na III awamu ya kwanza.

Kwa upande wake katibu tawala mkoa wa Morogoro, Mhandisi Emannuel Kalobero aliwahimiza waandishi wa  habari, kuelimisha wananchi hususani walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini kutumia vyema fursa hiyo adhimu iliyowekwa na serikali kupitia TASAF ili kasi ya kupambana na umaskini iendelee kuwa na mafanikio.

Alisema kwa kiasi fulani inaweza kusemwa mpango huo wa TASAF umesaidia kuinua uchumi wa nchi na kufikia uchumi wa kati kufuatia walengwa wengi kufikiwa ambao wamezitumia fedha zao katika kuanzisha miradi mbali na kujitegemea kiuchumi.

Pia alisema elimu hiyo isaidie kutoa nafasi kwa wale waliofanya vizuri kujiondoa kwenye mpango kwani mpango huo na kuwa kichocheo kwa wengine kuondoka na kupisha wenzao na kutambua kuwa sio kwamba wanatakiwa kuwem kwenye mpango kwa miaka yote.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

TMA yapongezwa kuimarisha ubora na usahihi wa taarifa za Hali ya Hewa

Spread the love  WAFANYAKAZI wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

7 wafa Ulanga, mbunge alia kutelekezwa na mawaziri, Tanroad

Spread the loveWatoto saba wamepoteza maisha na zaidi ya kaya 70 kukosa...

Habari Mchanganyiko

Bil 12.4 zimetumika ujenzi wa miradi wilaya ya Momba

Spread the love MKUU wa wilaya ya Momba mkoani Songwe Kennan Kihongosi...

AfyaHabari Mchanganyiko

Songwe katika mikakati ya elimu ya lishe kudhibiti udumavu

Spread the love  SERIKALI mkoani Songwe imejipanga kuendelea kutoa elimu ya lishe...

error: Content is protected !!